Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu
Na.Vero Ignatus. Arusha
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
Katika kuadhimisha siku ya walaji duniani inayo adhimishwa kila mwaka
machi 15 kila mwaka imetoa mafunzo kwa waalimu wanafunzi zaidi ya 300
katika chuo cha ualimu Monduli mkoani Arusha.
Akizungumzia Madhumuni ya kutoa
elimu hiyo Kaimu meneja wa Mamlaka ya mawasiliano kanda ya Kaskazini
Francis Msungu amesema ni katika jitihadha zilezile za serikali za
kuhakikisha kwamba inamlinda mlaji kwa kumpa elimu juu ya haki na wajibu
wawatumiaji wa huduma za mawasiliano kwaajili ya kuleta maendeleo.
Katika kuadhimisha siku ya walaji
wameitumia kutoa elimu juu ya haki, na wajibu wa watumiaji wa huduma za
mawasiliano kama sehemu ya walaji,tahadhari za kuchukua katika
mawasiliano hususani mitandao.
Msungu amesema kwamba walaji,ni
kundi kubwa la kiuchumi ambalo huwa linaadhirika na kuathiri maamuzi ya
kiuchumi yanayofanywa na mataifa na makampuni ya kibiashara.
“Sisi kundi hili la walaji ni
kundi lile ambalo maoni yetu huwa usual a to kusikilizwa kwa makini
katika maamuzi ambayo yanafanywa ya kiuchumi” alisema.
Kwa upande wake Mhandisi
Mwandamizi wa Masafa (TCRA) Jan Kaaya ametoa tahadhari kwa jamii
kutokuweka taatifa nyingi zinazowahusu kwenye mitandao kwani siku za
hivi karibuni kumekuwa na wimbi la uhalifu ambalo wanatumia mitandao
kufuatilia taarifa za watu.
Jan amesema ni muhimu kuhakikisha
unapoweka taarifa ako katika mitandao hii ya kijamii,usiweke taarifa
zako nyingi zinazomiwezesha mtu kuzitumia hizohizo katika kukudhuru wewe
mwenyewe.
Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya mawasilianoTanzania kanda ya kaskazini Julius Filex Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya mawasilianoTanzania kanda ya kaskazini Julius Filex amezungumzia
suala la uninuzi wa simu na kisema kuna sheria ya Mawasiliano ya
kieletroniki na posta ya mwaka 2010/ambayo inamtaka mnunuzi wa simu
kuhakikisha baadhi ya vitu kabla hajakabidhiwa simu.
Ahakikishe amepewa risiti,garantiibya mwaka mzima,auziwe simu ikiwa kwenue box lake,pia aangalie simu yake ni bandia ama la kwa kutumia *#06
Ahakikishe amepewa risiti,garantiibya mwaka mzima,auziwe simu ikiwa kwenue box lake,pia aangalie simu yake ni bandia ama la kwa kutumia *#06
Mhandisi Mwandamizi wa Masafa (TCRA) Jan Kaay akizungumza na waandishi wa habari.Picha na Vero Ignatus Blog.
Kaimu
mkuu wa chuo cha Ualimu Monduli Jesca Moiro akizungumza katika mafunzo
hayo kama mwenyeji wa wanafunzi waalimu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mwanasayansi wa Masafa kutoka Mamlaka ya mawasilianoTanzania kanda ya kaskazini (wa kwanza kulia) Julius Filex akizungumza na waalimu wanafunzi katika chuo cha ualimu Monduli ,(kushoto )Afisa kutoka (TCRA) Osward Octavian akionyesha vitabu ambavyo ni muongozo kwa watumiaji wa mawasiliano.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya washiriki ya mafunzo hayo yaliyoandaiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania( TCRA) nakufanyika katika chuo cha Ualimu Monduli mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.





No comments :
Post a Comment