Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe.
Godfrey Zambi akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya
kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Lindi katika kikao
kilichofanyika leo tarehe 17 Machi, 2018 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Lindi.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya
Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu (kushoto)
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Meja
Jenerali Projest Rwegasira (kulia) wakati alipowasili kwa ajili ya
kukagua miradi mbali mbali na ukarabati wa mabweni ya wafungwa leo
tarehe 17 Machi, 2018 Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya
Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Cosato Chumi akizungumza
wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya
Mkoa wa Lindi katika kikao kilichofanyika leo tarehe 17 Machi, 2018
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi,
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ndg. Rajab Bakari (kushoto) akifafanua
jambo pale kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama
ilipokuwa inakagua miradi mbali mbali na ukarabati wa mabweni ya
wafungwa leo tarehe 17 Machi, 2018 Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Mussa Zungu
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya
Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa kupokea na kujadili
taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Lindi katika kikao
kilichofanyika leo tarehe 17 Machi, 2018 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Lindi.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE
No comments :
Post a Comment