Mnamo mwezi Julai 2017, Kampuni ya
Progress rail Locomotives (PRL) ya Marekani ilileta vichwa vya treni 11
katika Bandari ya Dar es salaa kwa ajili ya kuviuza vyenye namba 9014,
9015, 9016, 9017, 9018, 9019, 9020, 9021, 9022, 9023 na 9024.
Tarehe 27 septemba, 2017
Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa aliteua kamati ya wataalamu kwa ajili kubaini kama vichwa hivyo
ni vipya au la.Wajumbe wa kamati hiyo walitoka chuo kikuu cha Dar es
salaam, TEMESA na shirika la Reli Tanzania (TRC).Kamati hiyo ilifanya
kazi hadi 15 oktoba, 2017 na kukabidhi ripoti kwa
Mheshimiwa
Waziri.Kamati ilibaini kuwa vichwa hivyo vya treni ni vipya.
Aidha tarehe 16 Oktoba, 2017
Mheshimiwa Wazirikwa mara nyingine aliteua kamati ya wataalamu wenye
taaluma mbalimbali wakiwemo wanasheria wahandisi na wachumi kwa ajili ya
kujadiliana bei ya kuvinunua vichwa hivyo.
Awali mwaka 2015,Serikali ilinunua
vichwa kama hivyo 13 vyenye namba 9001, 9002, 9003
,9004,9005,9006,9007,9008, 9009 ,9010, 9011, 9012 na 9013 kwa bei ya
dola za kimarekani Milioni 3,200,000 kwa kichwa kimoja.Kamati hivyo
ilifanya majadiliano ya bei na kufikia muafaka wa kununua kwa dola za
kimarekani milioni 2,400,000 kwa kichwa kimoja ambavyo ni pungufu ya
dola 800,000 kwa kila kichwa cha treni kulinganisha na bei ya vichwa
tulivyonunua awali,kwa maana hiyo kwa vichwa 11 serikali imeokoa dola
8,800,000.
Majaribio yatakuwa katika awamu
tatu.Kwanza ni ukaguzi kwa kuvitizama(visual inspection),pili ni
kuviwasha na kuvipa mizigo vikiwa havitembei(load box) na tatu ni
kufunga na kuvuta mzigo tani 700 toka Dar es salaam hadi Morogoro na
tani 1200 toka Morogoro hadi Kigoma na Mwanza.
Ununuzi wa vichwa hivi 11
utaongeza ufanisi wa shirika kwani kwa sasa hivi tunavyo vichwa 29
madhubuti kati ya vichwa 47 tunavyovihitaji ili kutoa huduma nzuri kwa
wateja wetu.
No comments :
Post a Comment