Msanii wa muziki wa asili,
Mrisho Mpoto ambaye amekuwa kioo cha jamii kwa muda mrefu kutokana na
kutoa nyimbo za kijamii zenye kuwataka wananchi kuwa wazalendo kwa
kufanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato cha halali, kukemea rushwa
na uonevu, Ijuma hii amefurahishwa na Programu ya Umilikishaji Ardhi
(Land Tenure Support Programme – LTSP).
Programu hiyo ambayo
inatakelezwa katika Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani
Morogoro chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi chini
ya Waziri wake, Mhe. William Lukuvi ili kukabiliana na migogoro ya
ardhi ambayo imekuwa ikiibuka katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Programu hii ni mahsusi kwa
wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi ambapo takribani vijiji 160
vitanufaika. Hadi sasa, Programu imehakiki na kupima vipande vya ardhi
84,795 katika vijiji 40 vya Wilaya za Kilombero na Ulanga.
Kati ya vipande vilivyohakikiwa na kupimwa, jumla ya Hati za Hakimiliki ya Kimila 24,650 zimeandaliwa.
Mpoto ambaye amekuwa akitembea
katika maeneo mbalimbali ya nchi kusoma mazingira na kuwasikiliza
wananchi wanasema nini juu ya maisha yao ili anapoandika nyimbo zake
ziwe na kero za wananchi ambazo amezishuhudia kwa macho yake, wiki hii
alipita mkoani Morogoro na kuzungumza na wananchi kuhusu maisha yao
ndipo lilipo ibuka suala la programu ya Umilikishaji Ardhi (Land Tenure
Support Programme – LTSP).
Mshairi huyo amesema baada ya
kuzungumza na wananchi kadhaa ambao wamepitiwa na Programu hiyo
aligundua nyuso zao jinsi zilivyokuwa na furaha baada ya kukabidhiwa
hati zao ambazo zimeongeza thamani zaidi ya ardhi yao (viwanja na
mashamba) kwa kuwa tayari vinatambulika kisheria.
“Kwa miaka mingi nchi yetu
imekua na migogoro ya ardhi kati ya mtu na mtu,kijiji na Kijiji,
wakulima na wafugaji, hata wawekezaji na wana nchi, Wizara ya Ardhi
kupitia Mpango wa Land Tenure Support Programme (LTSP) inayotekelezwa
katika Wilaya Tatu za Kilombero, Ulanga na Malinyi baadae kusambazwa
Nchi nzima imefanya kazi kubwa sana,” alisema Mrisho Mpoto.
“Binafsi kama kawaida yangu
kuzunguka kila koja na nchi yangu na kuzungumza na wananchi, nimeona
ukubwa wa hii Programu, imeona thamani ya hii programu, wananchi
wanaongea kwa furaha ya hali ya juu kutokana na hii programu. Mimi sio
msemaji wa serikali lakini wakati nikiwa katika harakati za kutembea kwa
ajili ya shughuli zangu za sanaa huwa napata fursa ya kuongea na
wananchi wa eneo husika, wakazi wa Morogoro wanaishukuru sana serikali
pamoja na Waziri Lukuvi, naamini hii programu inaweza kuwa mwarobaini
wa haya matatizo ya ardhi, maana kila kipande cha ardhi kitapimwa na
mwananchi kupewa hati yake ya umiliki, naamini itaweza kuondoa kabisa
migogoro ya nrdhi nchini Tanzania, hongera Mhe.Lukuvi,” aliongeza Mpoto.
Alisema bado ataendelea kutembea
katika maeno mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kukutana na mashabiki wake
wa muziki na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ya nchi na pale
ambako ataona kuna haja ya kutoa msaada atawasiliana wahusika kwaajili
ya kutatua kero za wananchi.
Kazi nyingine zilizotekelezwa na
programu ya LTSP ni pamoja na kusimika alama za msingi 54 za mtandao wa
kijiodesia katika Wilaya za Kilombero, Ulanga, Malinyi na Mufindi,
Kupima mipaka ya vijiji 121 na kutatua migogoro 71 ya mipaka ya vijiji
iliyodumu kwa muda mrefu, Kuandaa vyeti vya Ardhi ya Kijiji kwa vijiji
57, Kuandaa mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji kwa vijiji 53 na
Kuchangia katika ujenzi na ukarabati wa masjala za ardhi na ofisi za
vijiji katika vijiji 61.
Viongozi wengi wa Wizara
wanaitembelea programu hiyo mara kwa mara na uongozi wa Wilaya na
wananchi wanatoa ushirikiano mkubwa sana kwa kuwa programu iko katika
Wilaya zao.
Hivi karibuni Katibu Mkuu Bibi.
Dorothy Mwanyika mara tu baada ya kuteuliwa na Mhe Rais kuwa Katibu Mkuu
wa Wizara alitembelea programu hiyo na kujionea namna programu
inavyotumia teknolojia ya kisasa kabisa kupima ardhi ya wananchi
vijijini. Pia, Mhe Naibu Waziri Mhe. Angelina Mabula nae alifanya ziara
katika eneo la programu.
No comments :
Post a Comment