Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla
ya uchangiaji wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyofanyika
jana usiku katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine
Shigela akimkabidhi Makamu wa Rais zawadi mara baada ya kumalizika kwa
zoezi la uchangiaji jana kwenye hotel ya Golden Tulip jijini Dar es
Salaam
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana aliwezesha kupatikana
kwa shilingi bilioni moja na milioni mia saba kwa ajili ya ujenzi wa
Hospitali ya Wilaya ya Muheza.
Katika hafla hiyo iliyofanyika
kwenye hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam, Makamu wa
Rais
aliwapongeza uongozi wa Wilaya ya Muheza na mkoa wa Tanga pamoja na
wananchi kwa kuamua kujenga hospitali yao ya wilaya ili kuboresha hali
ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Makamu wa Rais alisema Serikali ya
Awamu ya Tano imedhamiria kuimarisha ubora wa huduma za afya ikiwa ni
pamoja na kupunguza idadi ya vifo vya watoto kutoka kiwango cha vifo 66
kati ya vizazi hai 1,000 hadi kufikia kiwango cha angalau vifo 40 kati
ya vizazi hai 1,000. Aidha, Serikali imedhamiria kupunguza vifo vya
wanawake wajawazito kutoka 556 kwa mwaka 2017 katika vizazi hai 100,000
hadi kufikia 292 ifikapo mwaka 2020.
Sambamba na hilo Serikali kwa
kushirikiana na Wadau wa Maendeleo tuna mkakati wa kujenga, kukarabati
na kupanua miundombinu ya Vituo vya afya 208 ili kuimarisha utolewaji wa
huduma mbalimbali za afya.
Makamu wa Rais ameutaka Uongozi wa
mkoa pamoja na wa Wilaya ya Muheza kuupa kipaumbele mradi huu wa ujenzi
wa hospitali ya wilaya na kuhakikisha wanaweka mradi huu katika bajeti
zinazokuja pamoja na kutafuta wahisani wengine wa ndani na nje ya nchi
ili kuwezesha ujenzi wa hospitali hiyo kukamilika kwa haraka.
Makamu wa Rais aliwashukuru Wadau
wote walioshiriki na kuomba kila mmoja wetu achangie kwa uwezo na nafasi
yake ili hospitali ya Wilaya ya Muheza ikamilike mapema.
Mbunge wa Jimbo la Muheza Mhe.
Adadi Rajabu alimshukuru Makamu wa Rais kwa kuwezesha kufanikisha
kupatikana kwa mchango mkubwa ambao hawakuutegemea na kuahidi ili
kuuenzi mchango huu na mapenzi ya Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa wana
Muheza basi watahakikisha hospitali hiyo au jengo lolote lile la
Hospitali hiyo linapewa jina la Mheshimiwa Makamu wa Rais.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo pamoja na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
No comments :
Post a Comment