Wednesday, March 21, 2018

TAARIFA YA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM KUHUSU TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWA AFISA UBALOZI WA SYRIA.

MAKO
Mkuu wa Mkoa   na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda
IMG-20180321-WA0000
Afisa Ubalozi wa Syria ambaye taarifa zilizagaa mitandaoni zikidai ameshambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha  Jijini Dar Es Salaam. Taarifa hizoo zimeenda mbali zaidi na kusema kwamba Dar Es Salaam sio salama na kueleza watu wawe makini zaidi.
……………………………………………………………………………….
Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam nimeshtushwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Afisa Ubalozi wa Syria ameshambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha leo mchana Jijini Dar Es Salaam. Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kwamba Dar Es Salaam sio salama na kueleza watu wawe
makini zaidi.
Nawaomba sana wananchi wa Dar Es Salaam muendelee kuwa watulivu na mkielewa kwamba Mkoa wenu ni salama salama sana. Vyombo vya usalama vinalifanyia kazi tukio hili na taarifa za awali nilizopokea zinaonyesha tukio hili linaweza kuwa limepangwa na watu wa ndani. Tunafuatilia zaidi kujua kwa nini Afisa huyo hakuomba ulinzi wa polisi akiwa amebeba kiasi hicho kikubwa cha fedha na pia kwa nini dereva wake amekimbia.
Kwa hali ilivyo mpaka sasa kuna uwezekano ikawa ni tukio la kupangwa na watu wa ndani. Hatutaruhusu watu wachache wachafue taswira ya Mkoa wetu.
Uchunguzi ukifikia sehemu nzuri taarifa rasmi itatolewa na vyombo vyetu vya usalama. Ulinzi na usalama wa wananchi wetu ni muhimu sana.
Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam

No comments :

Post a Comment