Watu wawili wamekufa
wilayani Kasulu mkoani Kigoma katika ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba lililokuwa likitokea
wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea
kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha
gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.
Gari la Mkurugenzi
Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa
na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu
wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka
salama na hali zao ni nzuri.
Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.
No comments :
Post a Comment