Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria
Prof. Palamagamba Kabudi akisign kitabu cha wageni alipofika eneo ambalo
ujenzi wa Mahakama Kuu unafanyika
Waziri mhe. Prof. Palamagamba
Kabudi akisikiliza maelezo ya awali kuhusiana na mradi wa ujenzi
Mahakama Kuu mkoani Mara unaoendelea mjini Musoma
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi akizungumza kitu baada ya kutembelea na kujionea
maendeleo ya ujenzi wa Mahakama hiyo mjini Musoma
Prof. Kabudi na timu aliyoambatana nayo akizungumza na mkuu wa Wilaya ya Bunda kuhusiana na Mahakama ya wilaya hiyo
Prof. Kabudi akizungumza na kinana
wa kitanzania ambaye ni mtaalamu wa quantity surveyor ambaye
anajumuisha timu ya wataalamu wanaojihusishs na ujenzi wa jengo hilo
……………………
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba ametembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama Kuu mkoani Mara na
kujionea ujenzi huo unavyoendelea mjini Musoma
Akizungumza baada ya kupata
taarifa fupi kuhusu ujenzi wa Mahakama hiyo na kuutembelea
Prof. Kabudi
amewataka wasimamizi wa mradi huo kuutangaza kwani uwepo wa Mahakama Kuu
mkoani Mara kutaleta ahueni kubwa kwa wananchi wa mkoa huo ambao
walikuwa wanalazimika kwenda Mwanza kutafuta haki zao.
Mhe. Waziri amesema Mahakama hiyo
itakapokamilika wananchi wa mkoa wa Mara watapata haki zao kwa wakati
ndani ya mkoa wao bila ya kulazimika kwenda umbali mrefu kutafuta haki.
Ujenzi wa Mahakama Kuu mkoani Mara
unatekelezwa kupitia mpango mkakati wa miaka mitano wa Mahakama wa
2015/2020 ambao unatoa kipaumbele kwa ujenzi wa miundombinu ya Mahakama
nchini ili kusogeza huduma za Mahakama karibu na wananchi
No comments :
Post a Comment