- UTANGULIZI ;
Zipo taarifa kuwa baadhi ya
wananchi Mkoa wa Mjini Magharibi wanatumia, wanashiriki, wanafadhili au
kusaidia biashara ya madawa ya kulevya kama ilivyo kwenye maeneo mengine
nchini.
Hata hivyo Serikali ipo kwenye
vita kali ya kupambana na mtandao wa madawa ya kulevya na Inspekta
Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Kamisheni ya Polisi Zanzibar
waliunda timu kutoka Kitengo cha Operesheni Maalum za Polisi Makao Makuu
Dar es salaam kuja kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa kero hii kama
ilivyo kwenye maeneo mengine ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.- MATOKEO YA OPERESHENI ;
| S/N | MAFANIKIO | MATOKEO / IDADI |
| TAARIFA ZA INTELIJENSIA | ||
| Kupatikana kwa taarifa za watuhumiwa wanaojihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya (kutumia, kuuza, kufadhili au kusaidia) | 105 | |
| JUMLA KUU | 105 | |
| WATUHUMIWA WALIOPATIKA NA HATUA | ||
| Watuhumiwa waliofikishwa Mahakamani | 26 | |
| Watuhumiwa waliopo chini ya Upelelezi | 16 | |
| Watuhumiwa waliopo chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee) | 16 | |
| JUMLA KUU | 58 | |
| VIELELEZO | ||
| Heroin | Kete 1293 na Vifuko 3 sawa na Gramu 74.385 | |
| Banghi (Vifurushi) | 373 | |
| Banghi (Vifuko) | 3 | |
- WITO :
Natoa wito na tahadhari kwa
wananchi wote wanaohusika kwenye mtandao huu kuacha mara moja kwa kuwa
vita hii imeshaanza na inaendelea kwa lengo la kuhakikisha usalama wa
vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo maana madawa haya yanaathiri zaidi
vijana ambao ndiyo muhimili na nguvu kazi ya Taifa.
Aidha nawapongeza wananchi wote
waliotoa ushirikiano wa kutoa taarifa za uhalifu huu bila ya kuona
muhali. Niwaombe wananchi wote kuendelea na ushirikiano huu wa kutoa
taarifa.
Mwisho natuma salamu kwa
watuhumiwa wote waliotoroka kule walipo wajue kuwa wanatafutwa na
watakamatwa ili wahojiwe na hatimae kufikishwa Mahakamani.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza
Liberatus Sabas – DCP
Mkuu Wa Uperesheni Maalum za Polisi Tanzania
21.03.2018
No comments :
Post a Comment