Matukio ya Mkutano wa 65 wa
Mawaziri wenye dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi wanachama wa Jumuiya
ya Mashariki, kati na kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern
Africa Health Community, ECSA-HC), yanayoendelea jijini Dar es salaam,
yakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, kikao hicho kilifunguliwa juzi machi 19 na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitembelea Mabanda ya
LAB EQUIP LMTD na Banda la Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi TFDA
baada ya mapumziko mafupi ya Mkutano wa 65 wa Mawaziri wenye dhamana ya
Sekta ya Afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, kati na
kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health
Community, ECSA-HC).
Kikao cha ndani cha Mawaziri wenye
dhamana ya Sekta ya Afya katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki,
kati na kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health
Community, ECSA-HC), huku wakikubaliana kuimarisha utawala na kuweka
mikakati ya pamoja ya kudhibiti na kupambana na magonjwayanayolipuka
baina ya nchi hizo, pia
kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza kama vile
magonjwa ya Saratani, ambayo yanasababishwa na aina ya vyakula vyenye
mafuta kupita kiasi, matumizi ya vilevi na matumizi ya sigara.
Pia kuongeza uwajibikaji ili kuimarisha Sekta ya Afya hasa katika Afya ya mama na mtoto.
Picha Na Wizara ya Afya
…………………
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya
Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA
umemalizika leo jijini hapa kwa nchi wanachama kukubaliana maazimio
mbali mbali yanayolenga kutekeleza kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza
kama vile kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa.
Akizungumza wakati wa kufunga
mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu amesema makubaliano hayo yamelenga kuimarisha na
kuboresha sekta hiyo na afya ya wananchi kwa ujumla.
Aidha, Waziri Ummy amesema
kuwa wamekubaliana pia kuongeza uwajibikaji kwenye afya ya mama na
mtoto ili kuepusha vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
“Tumekubaliana kudhibiti
magonjwa yasiyoambukiza tumegundua katika nchi hizo magonjwa
yanayoongoza ni pamoja na kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya
mfumo wa hewa” alisema Waziri Ummy.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy
amesema kuwa Suala lingine walilokubaliana ni kutilia mkazo suala la
heshima kwa wajawazito kwa sababu mawaziri wameshauri pia Tanzania
kukitambua Chuo cha Upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini.
Waziri Ummy ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, amesema wamkubaliana wamekubaliana pia
kuimarisha ushirikiano na ulinzi katika maeneo ya mipaka.
“Kwa sababu nchi zina mipaka
lakini magonjwa hayana mipaka tukiimarisha itasaidia kuondoa na
kudhibiti uwezekano wa magonjwa hasa ya mlipuko kuenea ikiwemo Zika,
Ebola, Dengue, Chikungunya na mengineyo,” alisema Waziri Ummy.
Pamoja na mambo mengine,
Waziri Ummy amesema pia wamekubaliana kuimarisha masuala ya utawala
kwamba kila mmoja ana wajibu kwa nafasi yake kwani sekta ya afya ni
mtambuka.
“Tumeona kuna umuhimu mkubwa
wa kushirikisha sekta zingine ikiwamo kilimo, maji, elimu, utumishi,
mazingira zinahusika kwa ukaribu na masuala ya Afya” alisema Waziri
Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
azimio la saba walilokubaliana katika mkutano huo ni kuweka mkakati wa
pamoja kukabiliana na magonjwa akitolea mfano nchi ya Uganda ambao
wamepata ugonjwa wa Marbugy unaofanana dalili na ugonjwa wa Ebola.
Mkutano huo wa kujadili
masuala mbalimbali ya afya yalijumuisha nchi 9 kutoka Nchi za Afrika
Mashariki, Kati na Kusini ECSA umefanyika nchini Tanzania kwa siku tatu.
No comments :
Post a Comment