Mkazi wa kata ya Kakonyo, Wilaya
ya Missenyi mkoani Kagera ambaye ni Katibu Mwenezi wa CCM Bwana Faraja
Kaijage akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi
Maliasili na Utalii jinsi alivyopigwa na kuumizwa na wafugaji wa nchini
Uganda kwa kosa la kukamata mifugo ya waganda iliyokula mazao ya
wananchi wa Tanzania katika kijiji hicho mwaka 2016
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii wakikagua mpaka wa Tanzania na Uganda katika eneo la mto kagera
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii wakipanda juu ya jiwe la mpaka
wa Tanzania na Uganda namba BP 30 katika kata ya Bugango wilaya ya Missenyi mkoani Kagera
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani
kutoka Wizara ya Ardhi Dkt. James Mtamakaya akiwaonesha Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii mipaka iliyopo kati
ya Tanzania na Uganda
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii wakipanda juu ya jiwe la mpaka
wa Tanzania na Uganda namba BP 30 katika kata ya Bugango wilaya ya Missenyi mkoani Kagera
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula (mwenye Tshirt
ya njano) akiongoza Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
Ardhi Maliasili na Utalii kushuka katika jiwe la mpaka wa Tanzania na
Uganda namba BP 30 katika kata ya Kakunyu wilaya ya Missenyi mkoani Kagera
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii wakiwa mbele ya jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda namba BP 30 katika kata ya Bugango wilaya ya Missenyi mkoani Kagera (Picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
……………..
Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Nape Nnauye ameishauli
Serikali kuboresha mipaka ya nchi kwa wakati ili kuondokana na migogoro
inayojitokeza mara kwa mara kufuatia uvamizi wa wahamiaji kutoka nchi
jirani.
Ameyasema hayo katika ziara ya
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii
ilipotembea mipaka kati ya Tanzania na Uganda Wilaya ya Missenyi upande
wa
Tanzania Mkoa wa Kagera na Wilaya ya Isingiro upande wa Uganda.
Nape amesema suala la kulinda
mipaka ni muhimu hivyo ni vyema serikali kupitia Wizara ya Ardhi
ikatenga fedha za kutengeneza barabara zilizoko mipakani ili kurahisisha
ulinzi na usalama wa mipaka yetu na kuwezesha wakazi wa nchi hizi mbili
kutambua mipaka ili kuepusha migogoro ya matumizi ya ardhi.
“Tumebaini kuwa kuingia kwa
wananchi wa Uganda hasa kuleta mifugo yao katika lanchi ya Missenyi
kunachangiwa na kutokuwepo njia maalumu na alama maalumu
zinazotenganisha kati ya nchi na nchi hivyo watu wanaingia kupitia
katika vichochoro visivyo rasmi na kuhatarisha amani kwa wakazi wa
mipakani alisema Nnauye”
Kamati hiyo pia ilifanikiwa kufika
katika vijiji vya Rwengiri, Bwenkoma na Bubale vilivyopo kata ya
Kakunyu na kubaini kuwa baadhi ya alama zilizowekwa mpakani zimepotea
hivyo wafugaji kutoka maeneo mbalimbali wanaendelea na shughuli za
ufugaji bila kujali sheria.
Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali
Denice Mwila amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama imekuwa ikikagua
mipaka na kutatua changamoto mbalimbali hivyo kama barabara
itatengenezwa katika mipaka yote ya Missenyi kazi ya kuwabaini waarifu
itakuwa rahisi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula amesema kuwa mpaka
sasa Wizara imepokea shilingi bilioni 4 za kuimarisha mipaka ambapo
fedha zitakazotumika kuimarisha mpaka wa Tanzania na Uganda ni shilingi
Bilioni 1.9 na shilingi Bilioni 2.1 kwa mpaka wa Tanzania na Kenya.
Aidha kupitia ziara hiyo ya kamati
Dkt. Mabula ametoa wito kwa wawekezaji ambao ambao wameshindwa
kuendeleza maeneo yao kuja kuyaendeleza kabla ya kuchukuliwa hatua za
kuyagawa maeneo hayo kwa watu wengine.
“Kuna watu waliomba maeneo
wakafuge lakini wameshindwa na baadhi wanayatumia kwa kazi ambazo
hazieleweki huku baadhi wakiomba kufugia lakini wanayatumia kwa ajili ya
kazi nyingine, nitawachulia hatua kama watashindwa kufanya kazi
waliyoomba alisema Mabula.”
Akitoa taarifa kwa kamati hiyo,
Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kutoka Wizara ya Ardhi Dkt. James
Mtamakaya amesema kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya mabadiliko ya utawala na kwamba mpaka wa Tanzania na Uganda
uliasisiwa na Uingereza na Ujerumani mwaka 1890, ulitafisiriwa mwaka
1902-1904 kwa kutumia marundo 15 ya mawe ambayo baadhi ya malundo hayo
yapo mpaka leo.
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya
Ardhi, Maliasili na Utalii, ikiwa katika tarafa ya Missenyi ilitembelea
kata za Kakunyu, Mutukula na vijiji vya Rwengiri na Lyengoma ambapo ni
eneo huria la ranchi ya Missenyi ambalo lilitengwa na serikali kwa ajili
ya ufugaji wa Ng’ombe katika ranchi hiyo na baadhi ya maeneo kuwa na
wakazi wachache.
Akizungumza na wajumbe wa kamati
ya Bunge mkazi wa kata ya Kakonyo, Wilaya ya Missenyi ambaye ni Katibu
Mwenezi wa CCM Bwana Faraja Kaijage amesema kuwa kuna changamato kubwa
katika mipaka hiyo, ambapo kwa kumbukumbu zake mnamo Disemba 19, 2016
alipigwa na kuumizwa na wafugaji wa Uganda kwa kosa la kukamata mifugo
ya waganda iliyokula mazao ya wananchi katika kijiji hicho.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Missenyi,
Kanali Dennis Mwila amesema kuwa kuna migogoro katika baadhi ya vitalu
huria vya Missenyi vilivyogawiwa mwaka 2006 inayosabishwa na ukosaji wa
uzalendo kwa viongozi kwa kuwauzia ardhi wahamiaji haramu na baadhi ya
vitalu kuleta mifugo aina ya Ng’ombe kutoka Uganda kwa malipo haramu.
Wilaya ya Missenyi ni Wilaya
ilianzishwa mwaka 2007 ambapo imepakana na nchi ya Uganda upande wa
Kaskazini, Wilaya ya Karagwe upande wa Magharibi na Wilaya ya Bukoba
vijijini upande wa Mashariki ambapo pia Wilaya ina tarafa mbili, vijiji
77 na vitongoji 352.
Aidha upande wa mpaka wa Tanzania
na Uganda Wilaya inapakana na Rakai na Isingiro zilizopo nchini Uganda
ambapo mpaka una kilomita 110.7 na 0.5 ya umbali huo upo katika maji ya
ziwa Viktoria.
Kwa upande wa idadi ya vituo
vilivyo rasmi vya kupita watu ni vinne ambavyo ni Mutukula, Kilahya,
Bugango na Kashenye na njia nyingine zisizo rasmi zipo mipakani
takribani 20 vilivyo jirani na mpaka huo.
No comments :
Post a Comment