Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter
Mshama akizungumza jambo wakati wa halfa ya uzinduzi rasmi wa chuo cha
ufundi stadi (VETA) kilichojengwa na kanisa la Mission to Unreached Area
Church (MUAC) lililopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Askofu mkuu wa kanisa la Mission
to Unreached Area (MUAC) Samwel Meena kulia akimpa maelezo mafupi Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wakati wa halfa ya ufunguzi wa
chuo hicho cha VETA,
Askofu mkuu wa kanisa la Mission
to Unreached Area (MUAC) Samwel Meena akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu uzinduzi wa chuo hicho cha ufundi stadi amabcho imejngwa
kwa ajili ya kuweza kuwasaidia vijana wanaotoka katika maeneo ya vijiji.
PICHA NA VICTOR MASANGU
………………..
VICTOR MASANGU, KIBAHA
KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais
wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa
viwanda hatimaye kanisa la Mission to Unreached Area Church (MUAC)
lililopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani limeamua kujenga chuo
cha ufundi stadi
(VETA) kwa lengo la kuwawezesha vijana wanaotoka
katika maeneo ya vijijini ili waweze kujifunza fani mbali mbali ambazo
zitawasaidia kupata ujuzi na kuanzisha viwanda vidogovidogo na kujiajiri
wao wenyewe.
Kauli hiyo ilitolewa na Askofu
mkuu wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC) Samwel Meena
wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa chuo hicho ambazo zimehudhuriwa
na viongozi mbali mbali wa dini, serikali pamoja na wageni kutoka nchini
Ujerumani ambao wanajiusisha na masuala ya kuwasaidia vijana kuwainua
kiuchumi kupitia makanisa.
Askofu huyo alibainisha kuwa
lengo kubwa la kuanzisha chuo hicho ni kutokana na kubaini kuwepo kwa
wimbi kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana hususan wale wanaoishi
vijijini na kujikuta wanashinda kutwa nzima bila ya kujishughulisha na
kazi yoyote , hivyo ana imani kuwepo kwa chuo hicho ni moja na ukombozi
mkubwa ambao utaweza kuwasaidia kuondokana na hali ngumu ya kimaisha
na kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Kibaha Assumpter Mshama ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za
uzinduzi huo amempongeza askofu kwa kujenga chuo hicho ambacho kitaweza
kuwa ni mkombozi mkubwa katika kuleta fursa za ajira kwa vijana kupitia
mafunzo ya fani mbali mbali pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo
ambavyo vitaweza kuwasaidia katika kujikwamua kiuchumi.
Assumpter alisema kwamba chuo
hicho kitaweza kuwaletea manufaa makubwa vijana ambao wataweza kupata
faida mbali mbali kutokana na kufundishwa fani mbali mbali ambazo
zitaweza kuwasaidia kuweza kujiajiri wao wenyewe pindi watakapomaliza
masomo yao.
“Kwa kweli mimi napenda kuchukua
fursa hii kwanza kumshikuru Baba Askofu kwani ameweza kufanya jambo la
msingi sana kwa kuweza kuona umuhimu wa kumuunga Mkono Rais katika suala
zima la uchumi wa viwanda na hawa vijana pindi wakimaliza wataweza
kupata fursa ya kuweza kuanzisha viwanda vyao vidogo vidogo na kuweza
kujikwamua na wimbi la umasikini,”alisema Assumpter.
Nao baadhi ya wanafunzi wa chuo
hicho akiwemo Michael Adam na Rehema Deogratias walisema kwamba
matarajio yao makubwa katika siku za usoni ni pindi watakapohitimu
mafunzo yao ni kuweka mikakati kabambe kupitia fani zao walizosomea kwa
ajili ya kuweza kufungua viwanda vidogovidogo kwa lengo la kuweza
kujiajiri wao wenyewe ili kuondokana na wimbi la umasikini.
Aidha wanafunzi hao waliiomba
serikali ya awamu ya tano kuweza kuwasaidia kuwawezesha katika kuwapatia
mitaji mbali mbali ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika
kufanyia shughuli zao mbali mbali ambazo zitawasaidia katika kuleta
mabadiliko chanya ya kimaendeleo na kuondokana na tabia ya kuwa
tegemezi.
No comments :
Post a Comment