Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoa
wa Kaskazini Pemba kushirikiana katika shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais ameyasema hayo
wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha Afya cha Huduma
ya Mama na Mtoto Shumba Vyamboni wilaya ya Micheweni mkoa wa
Kaskazini
Pemba.
Kituo hicho cha Mama na Mtoto cha
Shumba Vyamboni kitatoa huduma za Mama na Mtoto ambapo jumla ya
Wananchi 5,593 wakiwemo wanawake wenye uwezo wa kuzaa 1543 na watoto
chini ya umri wa miaka mitano 984 watapata huduma bora ya uzazi, lishe
na ustawi wa mama na mtoto.
Vijiji vitakavyofaidika na huduma
ya kituo hicho ni pamoja na Kibubunzi, Kikunguni, Mihogoni, Nyuma ya
Mti, Mgeninje, Utaani, Shumba vya Mboni, Uwondwe, Mamoja, Gombe, Uwaani
na Bule.
Katika ziara hiyo yenye lengo la
kuhimiza shughuli za maendeleo Makamu wa Rais alikagua ujenzi wa Skuli
ya Sekondari ya Micheweni pamoja na kumtembelea Muasisi wa Chama Cha
Mapinduzi Bi. Mrashi ambapo alimkabidhi mabati ya kuezekea nyumba yake
inayojengwa na wanachama wa chama cha Mapinduzi katika eneo la Sizini.
Mwisho Makamu wa Rais aliweka
jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM la Ukunjwi ambapo aliwaambia
wakina Mama kuwa mstari wa mbele katika kuonesha njia ya kuwa kiongozi
bora.
No comments :
Post a Comment