Tuesday, March 20, 2018

BENKI KUU YA DUNIA YACHANGIA MILIONI 300 KWA AJILI YA MRADI WA MAJI VIJIJI


6
Na Florah Raphael.
Benki kuu ya dunia kwa kushirikiana na Wizara ya maji na umwagiliaji Tanzania wamekutana leo jijini Dar es salaam kujadili miundombinu na miradi bora ambayo itawapatia watanzania maji safi na salama, ambapo tangu mwaka 2006-2017 katika mpango wa kuboresha vyanzo vya maji Tanzania imefanikikiwa kujenga miradi ya maji 1468 badala ya 10810 na vituo vya kuchotea maji 123,888 huku vinafofanya Kazi vikiwa ni 83331 na 38602 vikiwa havifanyi Kazi, katika mkutano huo benki ya dunia imeahidi kuchangia milioni 300 kwa ajili ya mradi wa maji vijijini.
Akiongea na vyombo vya habari naibu waziri wa maji na umwagiliaji amesema kuwa kutokana na mafanikio hayo bado kuna changamoto kubwa katika ujenzi wa miradi hiyo kwani wahandisi wengi ni kutoka nje ya nchi na hawayafahamu vizuri mazingira ya Tanzania hivyo inapelekea kujenga miradi mingi ambayo kwa badae inakuwa haina maji hivyo inabaki kuwa hasara.
Hata hivyo amekanusha kwamba siyo kwamba hawataki wahandisi wageni bali wanawataka kuwa na ushirikiano na wahandisi wenyeji kwani wao ndio wanaijua vizuri geografia ya nchi yao na wanafahamu wapi panatoa maji na wapi hapatoi maji hata wakati wakiangazi.
” siyo kwamba hatutaki waje nchini hapana lakini wanatakiwa kuwasikiliza wenyeji wao kwani wakija hapa nchini wao wanakuwa na sauti kuliko wenyeji” amesema. Kamwelwe.
Aidha amesema kuwa changamoto nyingine ni teknolojia hasa kwa vijijini kwani miradi mingi vijijini imekuwa ikiendeshwa kwa diezeli hivyo kugharimu watumiaji gharama kubwa na matokeo yake kushindwa kumudu na hatimaye kukosa kutumia maji yaliyo salama na kuendelea kutumia maji ya madimbwi ambayo ni hatari kwa afya zao na kueleza kuwa kwa sasa watabadilisha miundombinu hiyo na kuifanya iweze kutumia umeme wa jua.
Amesema pia Wizara imejipanga kuwa na Sera na sheria ili serikali iweze kutoa bajeti ili kuweza kuboresha miundombinu ya maji taka na kuweza kujenga mitambo ya kutibu maji taka ambapo ameweka wazi kwamba wafadhili mbalimbali wameanza kujitokeza kufadhi, benki kuu ya dunia imetoa pesa ambayo itatumika kujenga mtambo wa kutibu maji taka mbezi bichi, Wakolea wametoa pesa itakayojenga mtambo kama huohuo maeneo ya jangwani na Kurasini ambapo tayari mtambo huo umeshajengwa na umefadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika.

No comments :

Post a Comment