Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za
polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Simon Sirro mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa
nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akihutubia mara baada ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akipokea mifuko ya saruji zaidi ya elfu sita kutoka
kwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Tanga Cement Bw. Lawrence Masha jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
…………………………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro kuwachukulia hatua mara moja
askari polisi ambao wamekiuka maadili na taratibu za jeshi hilo katika
mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Rais ameyasema hayo
wakati wa kuwekwa kwa jiwe la msingi wa ujenzi wa
nyumba 36 za askari
polisi katika eneo la Mfikiwe, wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini
Pemba.
Makamu wa Rais alitoa pongezi kwa
Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa tulivu na yenye
amani pia alitoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad
Masauni kwa kusimamia vyema zoezi la ujengaji nyumba za Polisi.
Makamu wa Rais pia alitoa pongezi
kwa kampuni ya Twiga Cement kwa kutoa Saruji mifuko zaidi ya elfu sita
pamoja na kampuni za Shubash Patel kwa kuchangia vifaavingine vya
ujenzi.
Awali Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani Nchini Mhandisi Hamad Masauni alipongeza Jeshi la Polisi kwa
kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kusema yeyote
atakayevunja sheria achukuliwe hatua bila kujali wadhifa au umaarufu
wake.
Kwa Upende wake Mkuu wa Jeshi la
Polisi nchini ameahidi kufanya kazi kwa taratibu na sheria lakini pia
alitoa wasihi kwa wanasiasa wanaochochea vurugu kwani wao watachukuliwa
kama wahalifu na si wanasiasa.
Ziara ya Makamu wa Rais
imekamilika leo ambapo pia alitembelea Hospitali ya Abdala Mzee ambapo
alijionea vifaa vya kisasa vilivyowekwa na huduma bora zinazotolewa.
Makamu wa Rais pia aliweka mawe
ya Msingi katika ujenzi wa madarasa katika skuli ya sekondari ya Ali
Khamis Camp pamoja na ujenzi wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Ole.
No comments :
Post a Comment