Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akisaini kitabu cha
wageni mara baada ya kufika katika shamba la mpira la Kalunga, katika
Kijiji cha Mwaya, Kilombero mkoani Morogoro.
Wananchi wa Kijiji cha Mwaya
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (hayupo pichani).
]
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero ndugu.
James Ihunyo akizungumza katika mkutano wa Mhe. Naibu Waziri wa Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na wananchi wa Kijiji cha
Mwaya, Mkoa wa Kilombero.
Shamba la mpira la Kalunga ambalo ni malighafi kwa ajili ya kiwanda cha General Tyre na viwanda vingine vya plastic.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikagua mipaka
katika shamba la mpira la Kalunga, Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akionesha jinsi ya
kugema utomvu katika mti wa ampira.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiangalia mpira
unaozalishwa katika shamba la mpira la Kalunga,
Madarasa yaliyokuwa yakitumika
kufundishia katika kiwanda cha Mang’ula Mechanical and Mashine Tools
(MMMT) ambayo kwa sasa hayatumiki.
Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akikagua kiwanda
cha kiwanda cha Mang’ula Mechanical and Mashine Tools (MMMT).
…………..
Serikali inasisitiza ujenzi na
uendelezwaji wa Viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo
ya watu, hivyo tumedhamilia kuendeleza Viwanda vyote vilivyobinafsishwa.
#Wizara yangu itahakikisha mipaka
ya shamba hili la mpira la Kalunga lenye ukubwa wa ekari 1,536
linalindwa na kuendelezwa ili kusaidia wananchi wa kata Mwaya katika
ajira.
#Nchi yetu inapoteza zaidi ya
trilioni 3 kila mwaka kununua magurudumu kutoka nje ya nchi hivyo ni
lazima tuzalishe magurudumu yetu wenyewe kwa kutumia malighafi ya hapa
nchini na shamba hili ni jukumu letu sote kulilinda.
#Sehemu ya shamba hili imechomwa
moto, mpo hapa mnaishi na mnashuhudia mali ya Serikali ikiteketezwa
wakati hii ni mali yenu wenyewe mnatakiwa kulinda shamba hili ambapo
serikali imeipa jukumu shirika lenu la NDC kuliendeleza hivyo mtoe
ushirikiano wa karibu ikiwa ni pamoja na kulinda shamba hili.
#Nimetembea na kukagua mipaka yote
ambayo ipo katika shamba hili na kushuhudia baadhi ya waliovamia shamba
na kujenga na wengine kufanya shughuli zao binafsi, natoa rai kwa
waliovamia eneo hili la Serikali kutafuta mahala pengine mapema kabla
sheria haijachukua mkondo wake.
#Kazi ya Serikali ni kuweka karibu
huduma za kijamii kama Barabara, Afya, Elimu n.k na hii itawezekana kwa
urahisi kwa Viwanda kufanya kazi kwani Serikali itapata kodi kwa ajili
ya kuwezesha huduma za kijamii.
#Wale wote waliopewa Viwanda na
kushindwa kuviendeleza na wengine kuamua kutoa baadhi ya mashine na
mitambo tutawakata na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria.
#Kutokana na uharibifu na wizi wa
mali za kiwanda uliofanywa naagiza kukamatwa maramoja kwa aliyekuwa
Meneja wa Kiwanda cha Mang’ula Mechanical and Machine Tools (MMMT)
ndugu. Theofil Ngonyani ili kufanya upelelezi wa kina wa mitambo ya
kiwanda ilipopelekwa.
Imeandaliwa na Kitengo cha Habari,
WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI.
No comments :
Post a Comment