Wafanyakazi wa TBL wakipata mafunzo sambamba na burudani za vinywaji baada ya saa za kazi
Wafanyakazi wa TBL Arusha wakifutilia mafunzo
Wafanyakazi wa TBL Mwanza wakifuatilia mafunzo ya mahusiano na afya
TBL Moshi hawakubaki nyuma katika mafunzo hayo
TBL Mbeya nao walishiriki mafunzo na mijadala ya mahusiano
………………
Kampuni ya TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBev, imeitumia Siku ya Wapendanao kuandaa semina za wafanyakazi wake kuhusiana na masuala ya mahusiano katika familia,
zilizoendeshwa na wataalamu wa masuala ya Saikolojia na ushauri nasaha
kutoka taasisi mbalimbali za mafunzo nchini.Semina hizo zilifanyika
katika viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es
Salaam,Mwanza,Mbeya,Kilimanjaro na Arusha.
Kwa
kutumia kauli mbiu ya ‘Nogesha Upendo Valentine hii’wafanyakazi
walipata fursa ya kupata mafunzo,na kushiriki mijadala kuhusiana na mahusiano bora katika ndoa na familia sambamba
na changamoto mbalimbali zilizopo ,pia waliweza kupata majibu na
ushauri wa changamoto hizo waliokuwa wakiendesha mafunzo.
Meneja Mawasiliano wa TBL Group,Amanda Walter,amesema kuwa wameamua
kuitumia siku hii kusambaza upendo na furaha kwa wafanyakazi wa kampuni
kwa kuwapatia mafunzo ya kuimarisha mahusiano ya ndoa zao na familia
zao sambamba na kupata ushauri wa changamoto mbalimbali za kifamilia
wanazokabiliana nazo katika Maisha ya kila siku.
“Moja ya sera ya kampuni ni kuwapatia kipaumbele wafanyakazi wake kuhakikisha wanapata maslahi mazuri ya kuendeleza Maisha yao na familia zao sambamba na kuwapatia
mafunzo mbalimbali yanayohusiana na kuendeleza taaluma zao na mafunzo
ya kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku wanapokuwa nje ya kazi kama
ambavyo wamepatiwa mafunzo ya mahusiano yanayolenga kuimarisha upendo
ndani ya familia zao na mahali popote”alisema Walter.
Mhadhiri
Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dk.Chris Mauki,ambaye
alikuwa mmoja wa wakufunzi wa semina hizo alibainisha jinsi matatizo ya
kisaikolojia na mahusiano mabaya hakumuathiri
mhusika wa matatizo hayo pekee na mwenza wake au familia yake bali hata
mwajiri wake kwa kuwa mfanyakazi akiwa na msongo wa mawazo ni vigumu
kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta tija.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL Group walipohojiwa kuhusiana na mafunzo hayo,walishukuru kampuni kwa kubuni mafunzo mbalimbali ambayo yanawasaidia katika Maisha ndani ya maeneo ya kazi na katika Maisha yao ya kawaida nje ya sehemu za kazi.
TBL Group imekuwa ikiitumia
siku ya Valentine kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii.Mwaka jana
wafanyakazi wake kutoka mikoa yote vilipo viwanda vyake walishiriki
kusaidia na kutoa faraja kwa watoto wanaosoma kwenye shule za walemavu
No comments :
Post a Comment