Thursday, February 15, 2018

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AJIUZULU

        Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ( pichani ) amejiuzulu 

Taarifa zilizotangazwa na kituo cha televiseheni cha taifa hilo zimesema kuwa Waziri Mkuu huyo pia amewasilisha barua yake ya kujiuzulu Uenyekiti wa chama chake cha Ethiopia People's Demecratic front.

Pamoja na kwamba hakuna sababu rasmi zilizotolewa za kujiuzulu kwa Desalegn, habari za uhakika zinasema kuwa uhenda ni kufuatia kuepusha mgogoro wa kisiasa zaidi nchini humo ambapo kumekuwa na maandamano dhidi ya serikali katika maeneo yenye makabila makubwa nchini humo ya Oromia na Amhara.

Watu 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika maandamano ya upinzani.

Hailemariam Desalegn aliingia madarakani Agosti 2012, baada ya kufariki kwa kiongozi shupavu Meles Zenawi.

Uchumi wa Ethiopia umekuwa ukikua kwa kasi, na hatua hii ya Desalegn inatishia mustakabali wa baadaye wa taifa hilo

No comments :

Post a Comment