BOHARI ya Dawa (MSD) imeendelea kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa katika mfumo wa ununuzi, utunzaji na usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara (Supply Chain Management) na kupata Ithibati ya Kimataifa ya ubora ya daraja la juu inayojulikana kama ISO 9001:2015 ambayo itadumu kwa miaka mitatu (2018 - 2020).
Hatua
hiyo imekuja baada ya ukaguzi wa ubora wa huduma zinazotolewa na MSD
uliofanywa na kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED mweziAgosti 2017, na
kudhihirisha kuwa huduma zake zinafuata miongozoya ya juu ya kimataifa
katika utoaji wa huduma za mnyororo wa ugavi.
Akizungumzia
hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu
amesema kuwa hatua hiyo ya kupata ithibati ya juu ya Ubora ya Kimataifa
imethibitisha umahiri wa MSD na imeongeza chachu ya utendaji, ubunifu na
kuboresha masuala yote yanayo husiana na mnyororo wa ugavi ilikuwapa
wananchi huduma bora, zenye viwango, bei nafuu na kuwafikishia kwa
wakati.
Bwanakunu
ameongeza kuwa Ithibati hiyo inaonesha dhahiri ubora wa mfumo wa
ugaviwa MSD kwa wateja na wananchi kwa ujumla, na kueleza kuwa huduma za
MSD zinaendelea kuboreshwa zaidi kwani taasisi hiyo iko katika kipindi
cha maboresho ya kiutendaji kupitia mpango mkakati wake wamwaka 2017 -
2020.
Mara ya
kwanza MSD ilipataIthibatiya kimataifa mwaka 2013 (ISO 9001:2008) baada
ya kukidhi matakwa ya ubora kwa huduma zake za Ununuzi, tunzaji na
Usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na iliweza
kuishikilia ithibati hiyo kwa miaka yote bila kunyanganywa, kutokana na
kuonekana kuendelea kukidhi viwango vya ubora kila walipokaguliwa.
MSD
imekuwa miongoni mwa taasisi za kwanza nchini kupata ithibati ya ubora
ya kiwango cha ISO 9001:2015 kutokakiwango cha ISO 9001:2008 na
imethibitisha umahiri wa utendaji wake.
You might also like:
No comments :
Post a Comment