Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa
CCM wa mkoa wa Mwanza, Dkt. Anthony Diallo wakiwa ndani ya pantoni ya
Orion wakivuka ziwa Victoria kutoka Mwanza kwenda Kamanga wilayani
Sengerema kwa Ziara ya Kazi Februari 15, 2018. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole kuelekea
kwenye eneo inapojengwa hospitali ya Halmashauri ya Buchosa, Februari
15, 2018. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka watumishi wa umma watumie utalaamu wao vizuri na wafanye kazi
kwa uhakika na kwa kujiamini ili matokeo ya utendaji wao yaonekane.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi,
Februari 15, 2018) mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Mwanza
alipowasili mkoani hapa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku saba.
Waziri Mkuu amesema watumishi wa
umma wanatakiwa watumie utalaamu wao vizuri na wafanyekazi kwa
kujiamini pamoja na kuwa na taarifa za kutosha za idara wanazoziongoza
ili wananchi waweze kupata tija.
Pia amewataka watendaji kuacha
urasimu na wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji
wa miradi ya maendeleo inatumika ipasavyo.
“Msimamo wa Serikali ni
kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo watumishi wajiepushe
na vitendo vya rushwa na matumizi mbaya ya fedha za umma.”
Pia Waziri Mkuu amewataka
watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya
kusikiliza kero zinazowakabili hususani za ardhi na kushirikiana nao
katika kuzipatia ufumbuzi.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa
Mwanza, Bw. John Mongela alimueleza Waziri Mkuu kwamba atahakikisha
wanafanya kazi kwa bidii na fedha zote za miradi zinatumika kama
ilivyokusudiwa.
Hata hivyo Bw. Mongela
alizungumza kuhusu hali ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika mkoa
huo kuwa ni ya kuridhisha na imefikia asilimia 80, pia wameboresha
huduma ya mama na mtoto.
No comments :
Post a Comment