Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno akizungumza alipotembelea
kata ya Mapinga ,wilaya ya Bagamoyo wakati wa muendelezo wa ziara yake
anayoendelea nayo mkoani hapo kushukuru kuchaguliwa nafasi hiyo.(picha
na Mwamvua Mwinyi)
Aliyekuwa mgombea udiwani
kata ya Mapinga kupitia ACT Wazalendo uchaguzi mkuu uliopita ,Tabia Juma
akiongea baada ya kuhamia CCM wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM
Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno aliyoifanya wilayani Bagamoyo,pamoja na
hilo uongozi mzima wa ACT kwenye kata hiyo ulihamia CCM.
Baadhi ya wanachama wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bagamoyo wakimsikiliza mwenyekiti wa CCM
Mkoani Pwani ,(hayupo pichani) wakati alipokuwa amefanya ziara yake ya
kushukuru wilayani humo .(picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
Uongozi mzima wa
Chama Cha Act Wazalendo Kata ya Mapinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
akiwemo aliyekuwa mgombea udiwani Tabia Juma ,wamekihama chama hicho na
kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Viongozi hao
wameamua kuhamia CCM wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM mkoani humo,
Ramadhani Maneno aliyoifanya Kata ya Mapinga,Bagamoyo.
Akiwapokea viongozi
hao akiwemo Tabia, mwenyekiti Shaban Rashid na katibu mwenezi Omary
Kibanda, Maneno alisema kwa sasa wapinzani hawana tena nafasi .
Alisema ,kutokana na
ilani ya chama kutekelezwa vizuri na kuisimamia serikali katika
kuwaletea maendeleo wananchi kero nyingi zimepungua.
“Wapinzani
wameshaona kwenye vyama vyao kwa sasa hakuna wanachokifanya zaidi ya
kuwavuruga na kuwachanganya wananchi,” alielezea Maneno.
Alisema kuwa serikali inaendelea kutekeleza kwa vitendo yale yaliyoahidiwa lengo likiwa ni kuleta maendeleo.
Akizungumzia juu ya usimamizi wa miradi alisema chama kitaendelea kuisimamia serikali ili kuhakikisha miradi yote inakamilika.
Mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Bagamoyo, alhaj Abdul Sharifu alibainisha watahakikisha
wanasimamia ilani ili utekelezaji wa miradi uwe na mafanikio.
Mwenyekiti huyo
alisema , chama kimejipanga kuwatetea wananchi kwa kuondoa changamoto za
maendeleo kwa kushirikiana na watendaji wa serikali.
Katika ziara hiyo , Maneno alitembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Kerege na kuzindua matawi ya chama .
February 27 ,ataendelea na ziara yake kwenye Jimbo la Chalinze kwa ajili ya kushukuru kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo.
No comments :
Post a Comment