 |
| Mshindi
wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka
Bonus, Rajabu Saidi Yote (kulia), ambaye ni mkaazi wa Tandika Dar es
Salaam, akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo
inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja
Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156
wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo. |
 |
| Mshindi
wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka
Bonus, Tinna Sharon Masatu (kulia), ambaye ni mkaazi wa Mbezi Beach
akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa
na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa
Tigo, Woinde Shisael (katikati). Zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa
katika promosheni hiyo. |
 |
|
Mshindi
wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka
Bonus, Margareth Martin Hiza (kulia), ambaye ni mkaazi wa Ubungo, Dar es
Salaam akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo
inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja
Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156
wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo.
|
 |
| Add caMshindi
wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka
Bonus, Daniel Joseph Swai (kulia), ambaye ni mkaazi wa Iala, Dar es
Salaam akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo
inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja
Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Zaidi ya simu 900 bado
zinashindaniwa katika promosheni hiyo. |
 |
|
Baadhi
ya washindi zaidi ya 84 waliojinyakulia simu aina ya Tecno R6 katika
promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus wakiwa katika picha ya
pamoja na balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo,
Mina Ali (kati) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi.
Jumla ya washindi 156 wa simu tayari wamepatikana katika promosheni hiyo
ambapo zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa.
|
Wateja 156 wa Tigo wajinyakulia smartphone za TECNO R6 4G
Zaidi ya simu 900 na bonasi za internet bado zinashindaniwa!
Dar es Salaam, Februari 26, 2018 – ‘Kwa sasa mama yangu
anatumia simu ya kawaida ambayo haituwezeshi kuwasiliana kikamilifu kwa
njia ya mtandao. Kwa mfano siwezi kumtumia picha
za wajukuu wake. Ndio
maana nitampa zawadi ya simu hii mpya niliyoshinda kutoka Tigo leo ili
iturahisishie mawasiliano yetu na kumfanya awe sehemu ya ulimwengu wa
kisasa wa mawasiliano.’ Haya ni maneno ya Margareth Martin Hiza,
mfanyabiashara na mkaazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam ambaye aliibuka
moja wa washindi wa simu mpya za kisasa senye uwezo wa 4G aina ya Tecno
R6 4G katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na Tigo
Tanzania.
Wateja wa Tigo Tanzania wanazidi kupata faida lukuki ikiwemo
bonasi za hadi GB 1 bure kwa matumizi yao ya intaneti pamoja na fursa ya
kushinda mojawapo ya simu janja 900 ambazo bado zinashindaniwa katika
Nyaka Nyaka Bonus, promosheni murwa inayowazawadia wateja wa Tigo
wanaounua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu
iliyoboreshwaya *147*00#.
Akikabidhi zawadi kwa washindi wa wiki hii, Meneja Mawasiliano
wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa bado kuna zaidi ya simu 900 aina ya
Tecno R6 zenye uwezo wa 4G ambazo zinashindaniwa na wateja watakaonunua
vifurushi vya intaneti vya kuanzia TSH 1,000 kupiita menu *147*00#.
‘Washindi wetu wote 156 tuliowapata kufikia sasa wanatoka sehemu
mbali mbali za nchi, kwa hiyo ninawashauri wateja wetu kote nchini
washiriki ili wajishindie bonasi za data bure pampoja na mojawapo ya
simu zaidi ya 900 za Smartphones ambazo bado zinashindaniwa,’ Woinde
alisema.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.
No comments :
Post a Comment