Kamanda Razaro Mambosasa
aakizungumza na waandhishi wa habari katika kituo kikuu cha Polisi
jijini Dar es salaam wakati alipotoa taarifa ya kuhusu matukio
mbalimbali jijini Dar es salaam leo.
……………………………………………………………………………..
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam linamshikilia Rajabu Mohamed(25) ambaye anatuhumiwa
kujifanya Freemason na kisha kufanya kila aina ya ukatili kwa wananchi
hasa wanawake.
Akizungunza leo,Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Sar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa mtu
Huyo amekuwa akifanya matukio hayo kwa muda mrefu na sasa
wamefanikiwa
kumkamata.
Mtuhumiwa huyo amedaiwa kuwa kwa
muda mrefu amekuwa akifanya matukio ya kikatili kwa wanawake,kufanya
unyang’anyi wa mali na kutoa vitisho kwa anaowafanyia ukatili huo kuwa
wakitoa taarifa atawanyonya damu na kukata viungo vya sehemu za siri
huku akiwafanya kila aina ya unyanyasaji wa kijinsia.
Mambosasa amesema kuwa baada ya
kumhoji mtu huyo amekiri kufanya kila aina ya unyanyasaji ,kupora
fedha,kuchukua kadi za benki na kutaka namba za siri,kufanya matukio ya
ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake.
“Huyu mtu tumemuhoji anasema kwa
sasa ameacha,ukimuangalia sura yake ni ya binadamu lakini ni mnyama wa
hali ya juu kabisa kama mnyama wa Seronera .Amefanya mambo mengi ya
kishenzi.
” Tunaendelea na taratibu
nyingine na baada ya hapo atapelekwa mahakamani ili ajibu tuhuma za
makosa ambayo yanamkabili ,Sheria tunataka ichukue mkondo wake,”amesema
Kamanda Mambosasa.
No comments :
Post a Comment