Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Muhammed Bakari Kambi akipokea cheti cha kutambua mchango mkubwa
uliofanywa na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria kutoka
mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau tukio lililofanyika mapema leo Serena
jijini Dar es salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
Muhammed Bakari Kambi akiongea na wadau wa Afya na waandishi wa habari
katika kikao cha kupokea cheti cha kutambua mchango mkubwa uliofanywa na
Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Meneja wa Mpango wa Kupambana na
Kudhibiti Malaria nchini Dkt. Ally Mohamed akiwasilisha taarifa mbele ya
wadau na waandishi wa Habari katika kikao cha kupokea cheti cha
kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Serikali katika kupambana na
ugonjwa wa Malaria kutoka mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau tukio
lililofanyika mapema leo Serena jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau akijiandaa kumkabidhi cheti Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari Kambi
Wadau wa Afya wakifuatilia kwa
umakini taarifa ilokuwa ikiwasilishwa na Meneja wa Mpango wa Kupambana
na Kudhibiti Malaria nchini Dkt. Ally Mohamed (hayupo kwenye
picha)wakati wa kikao cha kupokea cheti cha kutambua mchango mkubwa
uliofanywa na Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Malaria
……………………………………………………………………………..
Na WAMJW-Dar es salaam.
SERIKALI ya Jamhuri wa Muungano
Tanzania imepata tuzo kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kutambua
mchango mkubwa uliofanywa katika jitihada ya kudhibiti Ugonjwa wa
Malaria nchini.
Akikabidhiwa Tuzo hiyo wakati wa
mkutano wa siku mbili ulioanza leo wa kujadili mafanikio na changamoto
katika kudhibiti Malaria,Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammad
Bakari Kambi alisema tuzo hiyo imetolewa kwa Serikali na Watanzania kwa
ujumla na Shirika hilo kanda ya Tanzania
Prof.Kambi alisema tuzo hiyo
imetolewa kwa kuanisha mchango mkubwa uliofanywa na Serikali wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania katika kuweka Mikakati,Rasilimali fedha na
kufanya kazi kwa ukaribu na wahisani mbalimbali katika kupambana na
Malaria
Prof. Kambi aliendelea kusema
kuwa ushiriki wa Tanzania katika tafiti mbalimbali ambazo zimechangia
katika udhibiti wa Malaria ikiwemo utafiti wa kutumia vyandarua vyene
viuatirifu vya kuzuia mbu pamoja na tafiti za awali za chanjo za
kudhibiti Malaria.
“Mafanikio mengine ni upungufu
wa Ugonjwa wa Malaria kutoka wagonjwa milioni 18 kwa mwaka 2008 hadi
wagonjwa milioni 5.5 kwa mwaka 2017.Pia Malaria imekua chanzo kikubwa
cha vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano hivyo kumekua na
upungufu kutoka vifo 112 kati ya watoto 1,000 mwaka 2005 hadi vifo 79
kati ya watoto 1,000 mwaka 2016”.Alisema
Aidha, kipengele kingine katika
vita dhidi ya udhibiti wa ugonjwa wa Malaria ni kwamba, Tanzania ndio
nchi pekee Barani Afrika kuwa na kiwanda kinachotengeneza vyandarua
vyenye dawa ya kudhibiti mbu aenezaye Malaria.
Naye,Kaimu Mwakilishi Mkazi wa
WHO, Dkt. Ritha Njau amesema tuzo hiyo imetolewa kwa Tanzania baada ya
kufanikiwa kupunguza maambukizi ya Malaria kwa kipindi cha miaka 10,
hivyo WHO imeona ni vema kutoa tuzo hiyo ikiwa ni katika kutambua
mafanikio hayo.
Wakati huo huo,Meneja Mpango wa
Kudhibiti Malaria Nchini Dkt. Ally Mohammed alisema hali ya maambukizi
ya Malaria nchini hivi sasa imepungua na kufika asilimia 7.3 ambapo
lengo ni kutokomeza malaria nchini.
Dkt. Ally Mohammed Alitaja mikoa
ya Kigoma, Geita na Kagera hali ya malaria bado ipo juu, hivyo mkutano
huo utaweza kujibu maswali kwanini mikoa hiyo maambukizi ya malaria bado
juu na kitu gani kifanyike ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.
No comments :
Post a Comment