Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi waliowahi kuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira wakati akiwa ziarani Mkoani Songwe na Mbeya kukagua shughuli za uchimbaji wa Madini, Leo 20 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-WazoHuru Blog
Baadhi ya wananchi waliowahi kuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko alipokuwa akizungumza jambo wakati akiwa ziarani Mkoani Songwe na Mbeya kukagua shughuli za uchimbaji wa Madini, Leo 20 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi waliowahi kuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira wakati akiwa ziarani Mkoani Songwe na Mbeya kukagua shughuli za uchimbaji wa Madini, Leo 20 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Songwe
Naibu
Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amewahakikishia
baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe na Wilaya ya Rungwe
na Kyela Mkoani Mbeya kuwa serikali inamalizia mchakato wa uhakiki wa
madeni yote ya wadai hivyo pindi itakapomaliza mchakato huo wadai wote
watalipwa madeni yao.
Naibu
Waziri, Mhe Biteko ametoa kauli hiyo leo 20 Februari 2018 akiwa
Kijijini Kapeta, Kata ya Ikinga Wakati akizungumza na wananchi waliowahi
kuwa watumishi wa Mgodi wa Kiwira waliosimamisha msafara wake wakati
akiwa ziarani Mkoani Songwe na Mbeya kukagua shughuli za uchimbaji wa
Madini.
Alisema
kuwa wananchi hao ndio walioiweka serikali ya awamu ya tano madarakani
hivyo serikali haina haiwezi kuwasahau ama kutosimamia haki yao bali
wanapaswa kuwa wavumilivu wakati serikali inajiridhisha na madeni hayo
kabla ya kuanza kulipa ili kuwa na uhakika na watu wanaostahili malipo
hayo.
“Watumishi
lazima tukubali kwamba madeni haya tumeyarithi hayakuwa ya serikali
bali yalikuwa ya muwekezaji sasa ili serikali iweze kuyalipa ni lazima
ijiridhishe isije ikaingia mkenge wa kulipa watu wasiostahili kwani
madeni hayo ni makubwa na yanahitaji kujiridhisha” Alisema Mhe Biteko na
Kuongeza kuwa
“Sisi
serikalini tunalifanyia kazi jambo lenu na tumeshafanya kazi kwa kiasi
kikubwa mpaka sasa ya kuona namna ya kuwalipa na ninataka niwahakikishie
kuwa kila mwenye haki anayedai lazima atalipwa lakini mtuvumilie
tumepita kwenye michakato mingi ya kuibiwa fedha kwa watu kupachika
madeni ya watu wasiostahili kulipwa tena wengine walishafariki”
Mhe
Biteko aliongeza kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli inatambua
kuwa mgodi wa Kiwira na mradi wa uchimbaji makaa ya mawe wa Kabulo ni
miradi ya kimkakati katika Wizara ya Madini hivyo inatambua umuhimu wake
na tayari ipo mbioni kuanzisha tena uzalishaji katika mgodi huo ambao
uzalishaji wake ulisimama tangu mwaka 2009.
Alisema
kuwa wananchi wamesubiri kwa muda mrefu malipo yao lakini tatizo kubwa
ilikuwa ni serikali kujiridhisha na kuanisha wanufaika wa madeni hayo
hivyo serikali italimaliza jambo hilo na itabaki kuwa historia.
Alisisitiza
kuwa katika maeneo mengi kulikuwa na changamoto mbalimbali lakini
tayari serikali imezipatia ufumbuzi changamoto hizo na wananchi wanaona
utofauti.
Akijibu
maswali ya wananchi hao waliotaka kufahamu ni lini mradi huo utaanza
uzalishaji, Mhe Biteko alisema kuwa ili mradi uweze kuanza zipo taratibu
za kisheria ambazo lazima zifuatwe ili yasijejitokeza matatizo ya
kisheria baadae hivyo zitakapomalizika haraka mradi huo utaanza
uzalishaji na wananchi watajipatia ajira.
No comments :
Post a Comment