Tuesday, February 20, 2018

DKT. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BODI YA UTALII (TTB)

 Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi
hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
…………………………………………………………………
Waziri
wa Maliasili na Utaliii, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo Februari 20, 2018,
amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Makao makuu ya Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) Jijini Dar es Salaam na kuitaka kufanya kazi kwa kasi na ubunifu
zaidi.
Akizungumza
na viongozi wa Bodi hiyo, Dkt. kigwangalla amewataka kuongeza kasi zaidi katika
kutangaza Utalii wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha studio ya kimataifa
ya kutangaza vivutio vya Tanzania ndani na nje ya nchi kwa kutumia lugha
mbalimbali za Kimataifa.
Aidha,amewataka
kuharakisha zoezi la uwekaji wa mabango yanayotangaza Utalii wa Tanzania katika
viwanja vya ndege hususani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar
es Salaam (JNIA).
Hata
hivyo amewataka pia kujikita zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii kwa
kuhakikisha inahuishwa mara kwa mara.
Pamoja
na hayo, ameiagiza bodi hiyo, kushirikisha wadau mbalimbali wanaotoa huduma za
Utalii ikiwemo madereva taxi na Marubani kwa kuwapa elimu ya kutangaza
utambulisho wa Tanzania kupitia Utalii na vivutio vilivyopo.
Akiwa
katika ofisi hizo ndani ya jengo la Utalii House, alikagua ofisi mbalimbali za
bodi hiyo pamoja na zile za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na
kupata maelezo machache kutoka wa maafisa wa Shirika hilo.
 Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na uongozi wa bodi
hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20 Februari, 2018.
 Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi hiyo, Devetha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema
leo tarehe 20 Februari, 2018.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi hiyo, Devetha Mdachi kukagua mazingira ya ofisi hiyo mapema
leo tarehe 20 Februari, 2018.
Picha
ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na uongozi
wa bodi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza mapema leo tarehe 20
Februari, 2018.

No comments :

Post a Comment