Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Equity, Joseph Iha akizungumza na
wageni waalikwa na wanahabari waliofika katika uzinduzi uliofanyika
jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking
inayomsaidia mteja kufanya miamala yake bila stress wakati wowote 24/7
popote atakapokuwa. Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG.
Wateja walihudhuria uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayotolewa na benki ya Equity jijini Dar es Salaam.
Wateja walihudhuria uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayotolewa na benki ya Equity jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Equity Joseph Iha (wa pili toka kushoto) akizungumza na wanahabari
jijini Dar es Salaam kutoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali mara baada
ya uzinduzi wa huduma ya Eazzy Banking inayomsaidia mteja kufanya
miamala yake bila stress wakati wowote 24/7 popote atakapokuwa. Pembeni
ni wakurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo ikiongozwa na Simbeye.
Picha/Habari: Cathbert Kajuna -Kajunason/MMG.
Benki ya Equity imezindua huduma
za kibenki kwa njia ya mtandao ambapo wateja wao sasa watapata huduma
mahali popote kupitia simu za mkononi, tablets na kompyuta za mezani na
mpakato.
Akizungumza Dar es Salaam wakati
wa uzinduzi wa Eazzy Banking, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Joseph Iha
amesema kuwa huduma hizo mpya zitatoa fursa kwa wateja kufanya miala
mahali popote.
Huduma hizo watazipata kupitia
Eazzy Banking kwa kufanya miamala kirahisi iwe usiku au mchana, wakiwa
nyumbani, au ofisini na kubwa zaidi sasa watakuwa na nafasi ya kuokoa
muda na gharama.
“Huduma za Eazzy Banking
zitaambana na EazzyBanking App, app ya kimataifa ya masuala ya kifedha
inayounganisha huduma za laini za simu na kuwawezesha wateja kutuma
fedha na pia kufanya malipo kupitia simu zao popote walipo na wakati
wowote.
“EazzyBanking ni rahisi kuianzisha
na hutoa huduma za kipekee kama kutuma fedha kwenda akaunti za benki
au mitandao ya simu, kuomba na kulipia mikopo , kulipia bili(ankara) na
aina ya huduma za malipo,” amesema Iha.
Amefafanua kwa wale wenye simu za
kawaida, kuna suluhisho kwao ambalo linajukulikana kama Eazzy24/7.
Huduma hiyo ambayo imeboreshwa inawezesha watumiaji kupata huduma
zilezile kama za EazzyBanking App kwa kupigiga *150*07# kupitia simu
zao.
Ameongeza ndani ya huduma hiyo
kuna kipengele cha huduma ambacho mtandaoni unaweza kufanya manunuzi ya
rejareja ambapo wateja wataendesha akaunti zao na hiyo inajulikana kama
EazzyNet; huduma ya malipo mbalimbali inayoitwa EazzyPay ambayo
huwezesha kufanya malipo ya bili kama ving’amuzi, Tanesco, Luku na
Dawasco.
Pia amesema inawezesha kununua na
kulipia bidhaa na huduma kupitia kwa wauzaji waliosajiliwa kama
Supermarket na hoteli kwa pale unapoona bango au stika ya “EazzyPay
inakubalika hapa”.
“Huduma ya mkopo kwa njia ya simu
inayoitwa EazzyLoan pamoja na uvumbuzi na usimamizi wa fedha kwa SMEs
/wafanyabiashara wa kati na wateja wakubwa, kampuni kubwa au Wizara kwa
kupata huduma kupitia EazzyBiz.
“Pia kuna EazzyKikundi ambayo hiyo
inatoa nafasi ya kusaidia Saccos, Viccoba, vikundi vya kiuchumi na
uwekezaji na utunzaji kumbukumbu za biashara,”amesema na kusisitiza
kupitia EazzyBanking wateja watapata huduma za kibenki kirahisi , salama
na bila stress, “amesema Iha.
Akifafanua zaidi amesema uzinduzi
wa huduma hiyo ya kibunifu unaongozwa na huduma mama ya EazzyBanking App
ambayo itaimarisha mbinu mkakati za kibenki katika kuwahudumia wateja
kimtandao kutokana na mabadiliko ya mahitaji yao.
Amewahakikisha Watanzania kuwa
benki hiyo ipo makini katika kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora
kwa wateja wake na kuomba wale ambao hawajajiunga na benki hiyo huu ndio
wakati sahihi kwani mambo yote ya kibenki unayafanya bila Stress.
No comments :
Post a Comment