Monday, January 29, 2018

MAADHIMISHO WIKI YA SHERIA 2018


IMG_1225 (5)
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi na Jaji Mkuu Prof.
Ibrahim Juma wakimalizia matembezi kuadhimisha kuanza kwa wiki ya
sheria nchini.
IMG_1229
Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi na Jaji Mkuu Prof.
Ibrahim Juma wakifanya mazoezi katika viwanja vya Mnazi mmoja
kuadhimisha kuanza kwa wiki ya sheria nchini.naomba kuwasilisha
………………
Waziri wa Katiba na Sheria  ameshiriki matembezi maalum  kuzindua rasmi maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini akiambatana na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma, Jaji Kiongozi Mhe. Faustin Rwambali, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome,Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju na Viongozi wengine wa Mahakama na Serikali.

Matembezi hayo yalianzia Makahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kupitia barabara ya Ohio, barabara ya Obama, Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Barabara ya Kivukoni, Kituo cha Kati cha Polisi , barabara ya Nkrumah, barabara ya Lumumba na kuishia Katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Maonyesho na utoaji wa huduma za kisheria kwa wananchi yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja  yakijumuisha Mahakama,Serikali na taasisi zake za kisheria na wadau wa sheria nchini wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini.
Maadhimisho hayo pia yanaambatana na michezo ya burudani ya soka baina ya timu ya Mahakama ya Tanzania, Bunge la Tanzania na Clouds Media Group.
Wizara inashiriki maadhimisho hayo ambapo inataraji kutoa elimu kwa umma juu ya shughuli mbalimbali inazofanya na kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wenye uhitaji

No comments :

Post a Comment