Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira akimsalimia
Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wakala wa Majengo nchini (TBA-B),
Manasseh Slekelaghe (Kushoto), mara baada ya Katibu Mkuu huyo kumaliza
ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za askari Magereza, zilizopo
Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katibu Mkuu huyo aliiagiza TBA
kumaliza ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano kuanzia sasa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira (wapili kushoto)
akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza,
Mhandisi Khadija Salum, alipokua anamuonyesha Katibu Mkuu huyo maeneo
mbalimbali ya ujenzi wa nyumba hizo zilizopo Ukonga, jijini Dar es
Salaam. Katibu Mkuu huyo aliiagiza TBA kumaliza ujenzi huo kwa muda wa
miezi mitano kuanzia sasa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira (katikati)
akimsikiliza Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Cosmas Mtambala
(kushoto), alipokua akimuonyesha Katibu Mkuu huyo hatua mbalimbali za
ujenzi wa nyumba hizo zilipofikia. Katibu Mkuu alifanya ziara ya
kuzitembelea nyumba hizo, zilizopo Ukonga,jijini Dar es Salaam,
kuangalia ujenzi unavyoendelea. Katibu Mkuu huyo aliiagiza TBA kumaliza
ujenzi huo kwa muda wa miezi mitano kuanzia sasa.
Moja ya jengo la Makazi ya Askari
Magereza likionekana hatua iliyofikia. Nyumba hizo zilizopo Ukonga
jijini Dar es Salaam, zinajengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA-B) na
kusimamiwa na Jeshi la Magereza nchini. Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, aliiagiza TBA,
kumaliza ujenzi wa nyumba hizo kwa muda wa miezi mitano kuanzia sasa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira akiwafafanulia
jambo wajenzi wa Nyumba za Askari Magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es
Salaam, ambao ni Wakala wa Majengo nchini (TBA-B). Kushoto (meza kuu)
ni Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam (TBA-B), Manasseh Slekelaghe,
anaefuata ni Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba hizo, Mhandisi Khadija
Salum, na kushoto ni Mhandisi wa Mradi huo, Peter Kikwati. Kulia ni
Msimamizi wa Mradi wa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la
Magereza, Cosmas Mtambala. Katibu Mkuu alizikagua nyumba hizo leo na
kutoa muda wa miezi mitano ziwe zimekamilika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Mstaafu, Projest Rwegasira akiwafafanulia
jambo wajenzi wa Nyumba za Askari Magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es
Salaam, ambao ni Wakala wa Majengo nchini (TBA-B), pamoja na wasimamizi
wa mradi huo ambao ni Maafisa wa Jeshi la Magereza. Kushoto (meza kuu)
ni Kaimu Meneja wa Mkoa wa Dar es Salaam (TBA-B), Manasseh Slekelaghe.
Katibu Mkuu alizikagua nyumba hizo leo na kuiagiza TBA kumaliza ujenzi
wa nyumba hizo kwa muda miezi mitano kuanzia sasa.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments :
Post a Comment