Taasisi
ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Profesa Jin
Sang LEE kutoka Chuo Kikuu cha New York – Korea (SUNY Korea) kwa
ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) waliandaa
mhadhara wa kubadilisha uzoefu ili kuweza kufikia malengo ya uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025.
Mhadhara
huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF na kufunguliwa na
Mheshimiwa Anthony Mtaka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Akizungumza katika
mhadhara huo, Mheshimiwa Mtaka alisema, nchi yetu imejipanga kufikia
uchumi wa kati kwa kuwa na sera na mikakati mbalimbali. Aliongeza kwa
kusema kilichobakia ni kuendelea kuitekeleza sera na mikakati hiyo ili
kutimiza ndoto ya kuwa na uchumi wa kati.
Kwa
upande wake, Dkt. Tausi Kida- Mkurugenzi Mtendaji ESRF alisema,
mhadhara huo umekuja wakati muafaka kwa kuwa nchi yetu imedhamiria
kufikia Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, ambapo sekta binafsi itakuwa
injini ya ukuwaji wa uchumi.
Profesa
Jin Sang LEE katika Mhadhara wake alianza kubadilishana uzoefu kwa
kuelezea mapinduzi ya uchumi katika Korea ya kusini kuanzia miaka ya
1960. Alisema katika miaka hiyo Serikali ya Korea ya Kusini iliweka
vipaumbele kadhaa ikiwamo kuondoa umaskini na kukuza viwanda. Katika
miaka hiyo serikali ilijikita katika uchumi wa viwanda vidogo vidogo na
wakijitahidi kuuza ndani na nje bidhaa ndogondogo. Katika miaka ya
sabini Korea ilipiga hatua nyingine kwa kupanua techonoljia ili kuongeza
tija katika viwanda vyake, Hayo yalikuwa yakifanywa kwa ushirikiano wa
serikali na sekta binafsi.
Katika
miaka ya themanini, nchi ilizidi kujikita katika sayansi, teknolojia na
ubunifu, waliweza kuwafundisha watu wake ili kuwa na wataalamu wengi
ambao watasaidia katika kubuni mambo muhimu ya maendeleo. Katika miaka
ya tisini, Korea Kusini ilinza kujikita katika kujiimarisha katika
teknolojia ambayo iliyohitajika kimataifa kama vile teknolojia ya
Tehama. Na katika miaka ya 2000, nchi ilieweza kuwa na mapinduzi makubwa
ya viwanda vya kubuni bidhaa mbalimbali kama vile simu za mikononi,
komptuta, magari n.k.
Hayo
yote ni matokeo ya uzalendo, kusomesha wataalamu, kuanzisha na
kusimamia masuala ya utafiti na maendeleo, kufanyakazi kwa bidii kwa
wananchi wa Korea Kusini. Masuala ya Utafiti na Maendeleo ni nguzo imara
katika kuendesha sekta mbalimbali katika nchi. Alisisitiza pia ,
ushirikiano kati ya serikali na vyuo vikuu amboko ndio sehemu ambayo
kutafumbuliwa na kukuzwa kwa sayansi, teknolojia na ubunifu.
Profesa
Lee alisema katika upande wa viwanda Tanzania inatakiwa kuwa na viwanda
vya msingi, masoko na kuwa na uelewa wa soko la kimataifa. Aidha kama
taifa linatakiwa kuwa na nadharia zinazofaa kwa ajili ya kubeba mfumo
huo wa viwanda kama
Pia
vyuo vikuu vinatakiwa kutengeneza wataalamu wa ngazi za juu watakaoweza
kusaidia sekta mtambuka kwenye masuala ya sayansi na teknolojia
kufanyakazi.
Aidha ameshauri serikali kujenga uwezo wa viwanda nchini kwa kuviwezesha kushindana huku ikitilia maanani soko la ndani na nje.
Katika
hilo inatakiwa kukuza ujasirimali kwa kuwezesha maarifa katika
menejimenti, kujiamini na kutengeneza ushirika na makampuni ya kigeni
Aidha
alihimiza uzalendo na kujitosa huku mtu akiwa na mawazo, maono na
mikakati ya kusonga mbele huku utekelezaji wa mambo kuelekea katika
ustawi wa viwanda ukiambatana na sera .
Profesa
Lee aliyasema hayo katika warsha ambayo ilijadili mafanikio ya Korea
Kusini katika viwanda na nini kinaweza kuigwa na watanzania kufikia
uchumi wa kati mwaka 2025. Alikuwa akizungumza kama mgeni mwalikwa
katika warsha iliyoshirkisha wataalamu mbalimbali nchini Tanzania kutoka
serikali na sekta binafsi
Akizungumzia
sekta binafsi alitaka, kuchukua pale ambapo serikali itakuwa imeishia
katika kutengeneza mifumo ya kuwezesha uchumi mkubwa kwa kuwa na
utaratibu wa kuwezesha sayansi, teknolojia katika kukuza shughuli zao.
Naye
mtaalamu wa Maendeleo ya Sekta binafsi Shirika la Umoja wa Mataifa la
Mpango wa Maendeleo (UNDP) Ernest Salla akizungumza wakati wa kufunga
warsha hiyo alisema kwamba ipo haja ya watanzania kuwa wazalendo na
kuhakikisha wanatimiza ndoto ya nchi ya viwanda kwa kuwekeza zaidi.
Aidha
alisema kutokana na kuwapo kwa maendeleo makubwa ya teknolojia na
sayansi Tanzania inaweza kutumia nafasi hiyo kusonga mbele kwa kasi
kuelekea sekta ya viwanda
Alitaka
kwa sasa sekta binafsi kuhakikisha inatumia fursa zilizopo kuleta
maendeleo badala ya kuwa na woga na hofu kutokana na vikwazo vya hapa na
pale.
No comments :
Post a Comment