Naibu
Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias
Kwandikwa (wanne kulia), Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack
(Mwenye ushungi) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (watatu kulia), jana
wakikagua miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kahama kabla ya
makabidhiano ya kurudishwa serikalini na Kampuni ya Madini ya ACACIA.Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainabu Telack akihutubia wananchi waliofika
kushughudia makabidhiano ya Kiwanja cha Ndege cha Kahama yaliyofanyika
jana baina ya Kampuni ya Madini ya ACACIA na Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA).Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Richard Mayongela (watatu kulia), akisaini nyaraka za makubaliano ya
kurudishwa Kiwanja cha Ndege cha Kahama kwa serikali kutoka kwa Kampuni
ya Madini ya ACACIA, ambapo wa pili kulia ni Meneja wa migodi ya
dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu, Bw. Benedict Busuzu na wakwanza kulia
ni Mwanasheria wa ACACIA, Bi Diana Wamuza, huku Naibu Waziri Sekta ya
Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa (mwenye miwani) na Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Bi. Zainab Telack wakishughudia.Mwanasheria
wa ACACIA, Bi. Diana Wamuza (wa kwanza kulia) akishuhudia makabidhiano
ya nyaraka za kurudishwa kwa Kiwanja cha ndege cha Kahama uliofanywa
jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA) na Meneja wa migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyahulu, Bw.
Benedict Busuzu.Naibu
Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias
Kwandikwa akizungumza mara baada ya makabidhiano ya kurudishwa
serikalini Kiwanja cha Ndege cha Kahama kutoka kwa Kampuni ya Migodi ya
ACACIA, uliofanyika jana mkoani Shinyanga. Mwenye ushungi ni Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga, Bi. Zainab Telack na wa kwanza kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Richard MayongelaNa Mwandishi Wetu, Kahama KAMPUNI ya madini ya ACACIA yenye kumiliki migodi ya dhahabu ya
Buzwagi na Bulyahulu imekirudisha serikalini Kiwanja cha Ndege cha
Kahama kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment