Dkt. Abbasi Aviasa Vyombo vya Habari Kuunga Mkono Mageuzi Yanayoletwa na Serikali
Mkurugenzi
wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati Jeupe) akimuonesha Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi Chumba cha kurushia matangazo wakati wa ziara yake ikiwa ni
sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona
utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akimsikiliza Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura (Mwenyeshati
Jeupe) wakati wa ziara yake yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa
kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo
Mjini Dodoma.
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Vyombo vya Habari nchini vimeaswa kuunga
mkono juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya
maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akizungumza Wakati wa ziara yake
yakutembelea Vyombo vya habari leo mjini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya
Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema
kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa wananchi
wanapata maendeleo endelevu kwa kuwa misingi ya Taifa letu imejengwa
katika uchumi jumuishi.
“ Kuna umuhimu kwa vyombo vya habari
kushiriki kikamilifu kueleza faida za miradi mikubwa ya maendeleo
inayotekelezwa kama ule wa ujenzi wa reli ya Kisasa (Standard Gauge) kwa
wananchi ili nao washiriki kikamilifu katika utekelezaji wake ambapo
ukishakamilika utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo” Alisisitza Dkt.
Abbasi
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiongea na wafanyakazi wa Radio ABM FM wakati wa ziara yake yake
ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili
kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.
–
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.
Hassan Abbasi akimkabidhi Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah Majura
(Mwenyeshati Jeupe) toleo Maalum la Jarida la Nchi Yetu kuhusu mafaniko
ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano.Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akifanya mahojiano maalum na Mkurugenzi wa ABM Fm Bw. Abdalah
Majura (Mwenyeshati Jeupe) wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya
utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi
wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.
Akifafanua amesema kuwa dhamira
yakuwaletea wananchi maendeleo inaendelea kutekelezwa kupitia mfumo wa
elimu bure, uzalishaji wa umeme wakutosha, Ujenzi wa uchumi wa Viwanda,
ujenzi wa miundo mbinu kama barabara, reli na upatikanaji wa huduma
muhimu kama madawa ambapo Serikali imeongeza bajeti ili kuhakiksha kuwa
kila mwananchi anapata huduma muhimu na za msingi katika ubora
unaotakiwa.
Aliongeza kuwa Serikali kwa sasa imeweka
msukumo na kipaumbele katika kutoa huduma bora kwa wananchi wote hali
inayotoa changamoto kwa vyombo vya habari kushiriki kikamilifu katika
kusaidia juhudi hizo ili malengo yake yafikiwe kwa wakati.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Radio ABM FM
wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea
vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini
Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiwa na Mkurugenzi wa RASI FM Bw. Ramadhani Mkosola (kushoto)
wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea
vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini
Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiongea na wafanyakazi wa Radio ya RASI FM wakati wa ziara yake
yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya habari
ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akifanya mahojiano maalum na kituo cha Radio cha RASI FM wakati
wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea vyombo vya
habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Radio ya RASI FM
wakati wa ziara yake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kutembelea
vyombo vya habari ili kuona utendaji kazi wa vyombo hivyo leo Mjini
Dodoma.
PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO
Katika kutekeleza majukumu yake Dkt.
Abbasi amepongeza vyombo vya habari kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta mageuzi ya kweli.
Aidha Dkt. Abbasi aliviasa vyombo vya
Habari kuzingatia weledi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku
ili kuchochea ukuaji wa uchumi na ujenzi wa Tanzania mpya kama ilivyo
dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari
MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali katika vyombo vya Habari Mkoani
Dodoma ni sehemu ya utaratbu wakutembelea wadau wa sekta ya Habari ili
kuimarisha utendaji kazi, ambapo Leo ametembelea vituo vya redio vya ABM
fm na RAS fm.
No comments :
Post a Comment