Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji wa
umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA
III) katika mkoa wa Tanga, watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijiji (REA) hawapo
pichani.
Wakandarasi wanaotekeleza miradi
ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini Awamu
ya Tatu (REA III)katika mkoa wa Tanga, watendaji kutoka Wizara ya
Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu
Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani)
……………………………………………………………………………………………………
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Nishati, Subira
Mgalu amesema kuwa wakandarasi walioshindwa kukamilisha miradi ya
usambazaji wa umeme vijijini Awamu ya Pili (REA II) watachukuliwa hatua
za kisheria na Serikali.
Mgalu ameyasema hayo tarehe 22
Desemba, 2017 katika ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es
Salaam katika kikao chake na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya
usambazaji wa umeme vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Tanga
inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini
Wakandarasi hao ni pamoja na
kampuni ya Derm inayosambaza miundombinu ya umeme katika wilaya za
Handeni, Kilindi, Korogwe na Lushoto, Kampuni za Radi, Njarita na
Aguila zinazosambaza umeme katika wilaya za Mkinga, Pangani, Muheza na
Bumbuli na kampuni ya Namis Cooperate Ltd inayosambaza miundombinu ya
umeme katika wilaya zote za Tanga.
Kikao hicho pia kilishirikisha
watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Naibu Waziri Mgalu, alisema kuwa
wakandarasi waliopewa kazi ya kusambaza miundombinu ya kusambaza umeme
vijijini kupitia REA Awamu ya Pili walilipwa malipo karibia yote hivyo
walipaswa kukamilisha miradi yote kwa wakati.
Aidha, aliwataka wakandarasi
wanaotekeleza miradi ya REA Awamu ya Tatu kuongeza kasi katika miradi ya
usambazaji wa umeme vijijini na kuongeza kuwa kipaumbele kitolewe
katika taasisi kama Shule, Vituo vya Afya, zahanati, Visima vya Maji ili
wananchi waanze kufurahia huduma za jamii.
Vilevile aliwataka wakandarasi
wanaotekeleza miradi ya REA katika mikoa miwili tofauti kuhakikisha kuwa
kasi inakwenda kwa kiwango sawa na kuepuka kuwekeza nguvu kwenye mkoa
mmoja tu.
“ Kwa wakandarasi wanaosambaza
miundombinu ya umeme katika mkoa zaidi ya mmoja lazima wahakikishe kasi
inakwenda sawa kwa mikoa yote, pasiwepo na mkoa ambao mradi wake
unakamilika mapema huku mkoa mwingine ukiwa nyuma kabisa,” alisisitiza
Mgalu.
Katika hatua nyingine, Naibu
Waziri Mgalu alitoa tahadhari kwa wakandarasi watakaobainika wanaingiza
nguzo za umeme na tranfsoma nje ya nchi tofauti na maelekezo
yaliyotolewa awali kuwa vifaa vyote vya ujenzi wa mradi wa umeme vitoke
hapa nchini
Alisema Serikali ilishakutana na
wadau wa vifaa ikiwamo wasambazaji wa Nguzo za Umeme na kiwanda cha
kutengeneza Transfoma cha TANALEC kilichopo jijini Arusha na
kujiridhisha uwezo wa wadau hao katika usambazaji wa vifaa.
No comments :
Post a Comment