Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa
shirika la madini la Taifa, (Stamico) Alexander Muganda akizungumza na
waandishi wa habari kwenye mnada wa madini ya Tanzanite uliofanyika mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander
Mnyeti akizungumza kwenye mnada wa madini ya Tanzanite uliofanyika mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Wadau wa madani ya Tanzanite
wakifuatilia mnada wa madini hayo uliofanyika mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Wadau wa madani ya Tanzanite
wakifuatilia mnada wa madini hayo uliofanyika mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na
Naibu Waziri wa Madini Ladslaus Nyongo (wapili kulia) wakizungumza
mawili matatu kabla ya kuanza kwa mnada wa madini kwenye mji mdogo wa
Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Wadau wa madini na askari polisi wakiwa
kwenye mnada wa madini ya Tanzanite uliofanyika mji mdogo wa Mirerani
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Kamishna wa madini nchini, mhandisi
Benjamin Mchwampaka akizungumza kwenye mnada wa madini ya Tanzanite
uliofanyika mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
……………….
Madini
ghafi ya Tanzanite yenye thamani ya shilingi bilioni 1.84 bilioni
yameuzwa kwenye mnada wa tatu wa kimataifa wa madini uliofanyika mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Kamishna
wa madini nchini, mhandisi Benjamini Mchwampaka akizungumza kwenye
ufungaji wa mnada huo alisema madini hayo yametokana na jumla ya gramu
47,201 zilizouzwa.
Mhandisi Mchwampaka alisema awali, kampuni tatu zilileta madini yao kuuzwa kwenye mnada huo lakini kampuni mbili zilijitoa.
Alitaja
kampuni hizo ni TanzaniteOne kwa kushirikiana na shirika la madini
nchini (Stamico) ambao wana ubia wa asilimia 50 kwa 50, kampuni ya
Tanzanite Africa na Clasic Gems.
Alisema
kampuni hizo zilileta madini hayo kwa ajili ya kuuzwa kiasi cha gramu
52,146.62 za madini ghafi ya Tanzanite na kampuni ya Classic Gems
ilileta karati 697.26 kwa ajili ya mauzo.
Alisema
kampuni mbili za Tanzanite Africa na Classic Gems zilijitoa kwenye
mnada huo baada ya kutoridhika na bei iliyotolewa hivyo madini
yaliyouzwa ni ya kampuni ya TanzaniteOne na Stamico.
Kamishna
huyo alisema Serikali inatarajia kulipwa shilingi milioni 128.7 za
mrabaha na ada ya ukaguzi na halmashauri ya wilaya ya Simanjiro
inatarajia kulipwa shilingi milioni 5 za kodi ya huduma.
“Kampuni
60 kutoka nchi saba za Tanzania, Marekani, Sri-Lanka, Hong Kong, India,
Thailand na China, zilishiriki kwenye mnada huo,” alisema mhandisi
Mchwampaka.
Mwenyekiti
wa bodi ya wakurugenzi wa Stamico, Alexander Muganda alisema mnada huo
wa kwanza umekuwa na mafanikio kama walivyotarajia.
“Tunashukuru
Rais Magufuli kwa agizo lake la kufanyia mnada eneo hilo la Mirerani
ambapo ndipo madini hayo yanapatikana,” alisema Muganda.
Naibu
Waziri wa Madini, Ladslaus Nyongo alisema serikali ya awamu ya tano
imeonyesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha kuwa rasilimali
zinawanufaisha watanzania kwa kiwango cha juu kabisa.
Nyongo
alisema tangu mwaka 2011 serikali ilianza utaratibu wa kutoa cheti cha
uhalisia kwa madini ya Tanzanite yanaposafirishwa kwenda nje kwa
utaratibu halali za serikali.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti alipongeza hatua ya kuweka mnada wa
madini ya Tanzanite sehemu ambayo yanachimbwa kama Rais John Magufuli
alivyoahidi.
Mnyeti
alisema serikali ya awamu ya tano itahakikisha inakusanya kodi kwa
wachimbaji wengine wa madini ya Tanzanite na siyo kuibana kampuni ya
TanzaniteOne pekee.
Mkuu
wa wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula alitoa shukurani nyingi
kwa Rais John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuagiza madini ya Tanzanite
yafanyiwe mnada kwenye mji mdogo wa Mirerani.
“Tunakumbuka
ahadi yake Rais Magufuli aliyoitoa wakati akizindua barabara ya lami ya
Kia-Mirerani kuwa minada yote ya madini ya Tanzanite yafanyike katika
machimbo haya ya Tanzanite na hilo limetekelezwa tunashukuru sana,”
alisema mhandisi Chaula.
Mkurugenzi
wa kampuni ya TanzaniteOne, Hussein Gonga alisema anashukuru uamuzi wa
Rais John Magufuli kuagiza mnada wa madini kufanyika eneo linalochimbwa
madini hayo.
Gonga
alisema jamii inayozunguka eneo hilo imenufaika kupitia mnada huo kwa
kufanya biashara mbalimbali kwa wadau wa madini ikiwemo nyumba za kulala
wageni, vyakula, vinywaji na mengineyo.
No comments :
Post a Comment