Na Florah Raphael.
Kampuni ya Viva Legency
inayohusika na mafunzo na ushauri elekezi imekuja na kitabu
kinachojulikana kama “Sote Tunaweza” kikiwa na lengo la kusaidia
harakati za mabadiliko pamoja na kukuza utamaduni wa mtanzania.
Akiongea na waandishi
wa habari Leo jijini Dar es salaam, Mtendaji mkuu wa Vivalegency
Fortunata Meela Temu amesema kuwa kitabu cha “Sote Tunaweza” kimeandikwa
kwa lugha ya kiswahili na kinampa msomaji uwezo mkubwa wa kubadili
fikra na kupiga hatua ya kimaendeleo.
“Kitabu cha sote
tunaweza kimeandikwa kwa lugha ya kiswahili na kinampa uwezo msomaji
kubadili kifikra na kupiga hatua kiamaendeleo” amesema Fortunata
Pia amesema kuwa katika
uandishi wa kitabu hicho wanetumia mifano ya watu mbalimbali kutoka
Tanzania na sehemu nyingine za dunia waliofanikiwa na kusema kuwa
wametumia mifano hiyo ili kumtia hamasa msomaji na kumfanya kufuata
nyendo za hao watu waliofanikiwa.
“Kitabu hiki tumetumia
mifano ya watu waliofanikiwa kutoka Tanzania na sehemu nyingine ili
kumpa msomaji hamasa ya kufuata nyendo zao” amesema Fortunata.
Pia Fortunata ameongeza
kuwa mafanikio yanaweza kupatikana kwa kuangalia fursa zinazopatikana
ndani ya jamii hivyo kuwataka watanzania kutumia lugha ya kiswahili kama
fursa kwa kuhabarishana na kuelimishana .
Kwa upande wake Naibu
katibu mkuu Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Dr.AveMaria Semakafu
ameipongeza kampuni ya Vivalegency na kusema kuwa kitabu cha “sote
tunaweza” kimekuja wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu ipo kwenye
harakati za mabadiliko kuelekea uchumi wa kati.
“Sote tunaweza kimekuja
wakati mwafaka kwa sababu nchi yetu IPO kwenye harakati za mabadiliko
kuelekea uchumi wa kati” amesema Dr.Semakafu.
Pia amebainisha kuwa
Tanzania inachangamoto kubwa katika utamaduni wa uandishi na usomaji
vitabu na kuwaomba watanzania watumie fursa ya kuandika vitabu vyenye
dhima yenye kuleta maana na kuachana na utamaduni wa kuandika vitabu
ambavyo havina dhima yoyote ya kubadili fikra na kuleta chachu ya
maendeleo.
No comments :
Post a Comment