Friday, December 22, 2017

TAASISI YA DR.AMON MKOGA FOUNDATION YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA WATU WENYE ULEMAVU NA VIKUNDI VYA KINAMAMA WA MKOA WA TABORA KUTOKA UBALOZI WA KUWAIT TANZANIA


002
Mwenyekiti wa Dr.Amon Mkoga Foundation, Bwana Amon Mkoga na kulia kwake ni Mhe.Stella Ikupa Naibu waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu akifuatiwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe.Jasem Al Najem, Ubalozi wa Kuwaiti umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora.
001
Mwenyekiti wa Dr.Amon Mkoga Foundation, Bwana Amon Mkoga na kulia Akizungumza na Waandishi wa habari ( hawapo pichani) Katika ni Mhe.Stella Ikupa Naibu waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu akifuatiwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe.Jasem Al Najem, Ubalozi wa Kuwaiti umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora.
003
Baadhi ya Misaada iliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora.
………….
Taasisi ya Dr.Amon Mkoga Foundation wamepokea msaada wa Vifaa vya watu wenye Ulemavu na Vikundi vya kinamama  wa  mkoa wa Tabora
-Wheel Chair Normal(Baiskeli za walemavu wakubwa)-15
-Wheel Chair For Infant(Baiskeli za walemavu wakubwa)-10
Crutches Elbow type pair(Fimbo za kutembelea)-10
-Crutches Elbow types pair(Fimbo za kutembelea)-10
-Walking stick brown(Fimbo za kutembelea )–10
-Stick for Blind(Fimbo za kutembelea vipofu)-20
-Spectacles for Blind people(Miwani ya jua kwa Albino)-15
-Sewing machines(kwa Walemavu na Wajane)-30
Katika Muendelezo wake Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe.Jasem Al Najem  katika kusaidia watu wenye ulemavu na mahitaji maalumu.

Kwa muda mrefu tumekuwakuwa tukishuhudia Ubalozi wa Kuwait ukisaidia makundi maalumu hapa nchini,hii itakuwa fursa kwa watu wenye ulemavu na vikundi mbalimbali vya kinamama kufaidika na mradi huu.
Kwanini msaada huu?kumekuwepo walemavu wengi wasiona uwezo wa kununu vifaa mbalimbali vya kuwasaidia hivyo kudumaza utendaji wao wa kazi,wajane pia watafaidika na msaada huu wa cherehani kwani migogoro ya ndoa  na vifo vya wenza imesababisha ongezeko la wajane katika siku za hivi karibuni.
Misaada hii italenga walengwa kutoka vijijini ambao hawana uwezo wa kununua vifaa hivi,baadhi ya Kata za Tabora ambazo wafaidika watatoka ni-
  • Chemchem
  • Cheyo
  • Gongoni
  • Ifucha
  • Ikomwa
  • Ipuli
  • Isevya
  • Itetemia
  • Itonjanda
  • Kabila
  • Kakola
  • Kalunde
  • Kanyenye
  • Kiloleni
  • Kitete
  • Malolo
  • Mbugani
  • Misha
  • Mtendeni
  • Ndevelwa
  • Ng`ambo
  • Ntalikwa
  • Tambukareli
  • Tumbi
  • Uyui
Tunashukuru mgeni Rasmi;Mhe.Stella Ikupa Naibu waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu kuja kushiriki nasi leo katika makabidhiano haya.
Waweza tembelea Tovuti yetu : www.dramonmkogafoundation.or.tz
Amon Mkoga
Mwenyekiti
0755-638 004/0655-638 004

No comments :

Post a Comment