Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akizindua miongozo ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Wafanyakazi mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi(WCF).
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akionyesha miongozo ya
utekelezaji majukumu ya baraza la wafanyakazi wa WCF kwa Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akizungumza kwenye kikao cha
baraza la wafanyakazi wa WCF.
…………..
Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde
ameendelea kukazia maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh
Jenister Mhagama aliyoyatoa kuwataka waajiri wote wawe wamejisajili
katika mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kwa kubainisha kwamba kwasasa
inaendelea operesheni maalum ya kuhakikisha maagizo hayo ya waajiri
kujisajili katika mfuko wa fidia yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria.
Mavunde ameyasema
hayo leo wakati akifungua Baraza la kwanza la Wafanyakazi wa mfuko wa
fidia kwa Wafanyakazi(WCF)katika makao makuu ya ofisi za WCF Jijini Dar
es salaam.
Amesema waajiri wote
nchini wanapaswa kutekeleza sharti la kisheria la kujiunga na mfuko wa
huo wa fidia ili kuilinda nguvu kazi ya Tanzania kutokana na
madhara/magonjwa yatokanayo na kazi na kuahidi kwamba atalisimamia agizo
la Waziri Mhagama kwa kuendesha operesheni ya ukaguzi nchi nzima
kubaini waajiri ambao bado hawajatekeleza takwa hilo la kisheria.
Naibu Waziri Mavunde amesema watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha, Mkurugenzi
Mkuu wa WCF Masha Mshomba amebainisha kwamba Mwajiri yoyote
atakayekutwa hajajisajili katika Mfuko atachukuliwa hatua kali za
kisheria ikiwamo faini isiyozidi Tsh.milioni 50 au kifungo cha miaka 5
Jela kwa Mkuu wa Taasisi husika au vyote kwa pamoja kama ilivyoainishwa
katika kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi No. 20 ya
Mwaka 2008..
No comments :
Post a Comment