Kamishna Jenerali wa Magereza,
Dkt. Juma Malewa akimkabidhi zawadi ya Sh. Milioni moja(1,000,000)
askari wa kike Sajini wa Magereza, Anna Akuny(katikati) kutokana na
utendaji wake mzuri kazini aliouonesha katika Gereza la Wanawake
Segerea(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza,
Gaston Sanga(wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza Segerea, ACP. Godfrey
Kavishe.
Askari wa Kike Sajini Anna
Akuny(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) mara baada ya kumkabidhi
zawadi ya utendaji kazi mzuri kazini. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa
Jeshi la Magereza, Makao Makuu.
…………………
Na Lucas Mboje, Jeshi la Magereza
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Dkt. Juma Malewa ametowa zawadi ya utendaji kazi mzuri kwa askari wa
Jeshi hilo Sajini Anna Akuny wa Gereza la Wanawake Segereza leo Desemba
5, 2017 katika Makao Makuu ya Magereza Jijini Dar es Salaam.
Askari huyo Sajini Anna
amekabidhiwa Sh. milioni moja (1,000,000) na Kamishna Jenerali wa
Magereza kutokana na kuonesha utendaji wake mzuri pamoja na nidhamu
kazini.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa amemtaka askari huyo
kutokubweteka na mafanikio hayo bali iwe chachu ya kufanya kazi kwa
bidii zaidi.
Jenerali Malewa ametoa wito kwa
Maafisa na Askari wa Jeshi hilo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria,
Kanuni, Taratibu na miongozo inayotolewa mara kwa mara na Uongozi wa
Jeshi hilo.
Hafla ya kukabidhi zawadi kwa
askari huyo imehudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza
Makao Makuu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, DCP. Augustine
Mboje pamoja na Mkuu wa Gereza Segerea, ACP. Godfrey Kavishe.
No comments :
Post a Comment