Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
NMB Ineke Bussemaker akimkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu fomu za Wajibu na Chipukizi
akaunti kwa ajili ya watoto wake kujiunga na huduma hiyo leo makao makuu
ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi Mwanafunzi wa
Darasa la Sita wa Shule ya Msingi Mlimani Latifa Ally zawadi ya
Madaftari katika makuu ya Benki ya NMB leo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa darasa la Sita wa
Shule ya Msingi Mlimani wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja
na viongozi wengine wa NMB mara baada ya kukabidhiwa zawadi na waziri
huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
NMB Ineke Bussemaker akifafanua aina mbalimabali za huduma ya benki yake
kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu leo makao makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa darasa la Sita wa
Shule ya Msingi Mlimani wakipata ufafanuzi wa matumizi ya akaunti ya
chipukizi kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo leo
jijini Dar es Salaam.
…………….
Na Anthony Ishengoma- Wizara ya Afya
Takwimu za Benki kuu ya Tanzania
zinaonesha kuwa asilimia 16 ya Watanzania kwa mwaka huu wamepata huduma
ya kibenki ukilinganisha na asilimia 9.1 ya mwaka 2006 ambapo asilimia
48 ya wananchi wamepata huduma za kifedha kutoka taasisi ndogo za huduma
za fedha pamoja na malipo kwa njia ya simu ikilinganishwa na asilimia
6.7 ya mwaka 2006.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hayo wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kufungulia watoto wao
akaunti maalumu ijulikanayo kama Wajibu, Chipukizi na Mwanachuo kwa
wanafunzi wa ngazi zote hapa Nchini kupitia mkakati mpya wa Benki ya NMB
ujulikanao pia kama uwezo wa kifedha.
Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa
kampeni hii ya uwezo wa kifedha inalenga kuhamasisha wanafunzi kote
Nchini kujiongezea uwezo wa kutumia huduma za kibenki na pia kujenga
nidhamu ya matumizi ya fedha na kujiwekea akiba kwa baadae kwa manufaa
ya elimu kwa watoto.
Aidha Mhe. Ummy ameiomba Benki ya
NMB kuhunganisha mpango wa huduma ya Toto Afya Kadi maarufu kama akaunti
ya elfu 50,400 na akaunti ya Wajibu ili wananchi wenye uwezo mdogo
waweze kuweka bima ya matibabu kwa watoto wao kwa kuweka fedha kidodo
kidogo ili kufikia kiasi kinachotakiwa kuanzisha bima ya afya ya mtoto.
‘’Wanachi wenye uwezo mdogo
wamekuwa wakiniambia kuwa wanapenda sana kushiriki katika mpango wa Bima
ya Afya ya mtoto yaani toto afya kadi lakini wamekuwa hawana uwezo wa
kulipa elfu 50,400 kama bima ya afya ya mtoto lakini kwa kupitia kampeni
ya uwezo wa kifedha ya akaunti ya Wajibu NMB itawawezesha wananchi hao
kulipa bima ya afya ya mtoto kwa kuweka kiwango kidogo kidogo,’’ amesema
Waziri Ummy Mwalimu.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji
wa NMB Ineke Bussemaker amesema kampani ya Wajibu ina maana ya
uwajibikaji ikiwa na akaunti tatu za akiba ambazo ni NMB mtoto akaunti
inayohusisha watoto chini ya miaka kumi na saba,Chipukizi akaunti ya
watoto miaka 13 mpaka 17 na NMB mwanachuo akaunti ya Wanafunzi wa elimu
ya juu.
Ameongeza kuwa NMB mtoto akauti
inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na mzazi wakati akaunti ya Chipukizi
inatoa uhuru wa vijana kumiliki akaunti yao ikiwa ni mara ya kwanza hapa
Nchini kwa vijana hawa kumiliki na kutumia ATM kadi kama ilivyo kwa
wazazi na walezi wao.
Uzinduzi wa kuhamasisha matumizi
ya akaunti hizi ni umezinduliwa leo jijini Dare es Salaam na Waziri
mwenye dhamana ya masuala ya Watoto mhe. Ummy Mwalimu pamoja na
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mlimani ambao tayari wanatumia huduma hii
ya kibenki baada ya kuwa wamehamisishwa na benki hiyo kutumia akaunti ya
Wajibu.
No comments :
Post a Comment