Ayman
Safadi alisema alimuambia waziri wa mashauri wa nchi za kigeni wa
Marekani Rex Tillerson kuwa hatua kama hiyo inaweza kuzua ghadhabu kubwa
kwa nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiisalmu.
Kuna uvumi kuwa Rais Donald Trump atatangaza hilo hivi karibuni na kutimiza ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni.
Jared Kushner, mkwe wa Trump alisema kuwa bado hakuna uamuzi uliofanywa.
Katika mtandao wa Twitter, Bw
Safadi alisema: #Nilizungumza na waziri Rex Tillerson kuhusu hatari ya
kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Hatua kama hiyo inaweza
kusababisha ghadhabu kwenye nchi za kiarabu na kwa ulimwengi wa kiislamu
na kuzua misukosuko na pia kuhujumu jitihada za amani.”
Hakuna jibu lolote kutoka kwa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani.
Naye rais wa Palestina Mahmoud
Abbas anajaribu kupata uungwaji mkono wa kimataifa katika kumshawishi
Trump asifanye tangazo kama hilo.
Ofisi yake ilisema kwa aliwapigia
simu Jumapili viongozi wa dunia wakiwemo rais wa Ufaransa Emmanuel
Macron na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
“Alitaka kulezea harari za uamuzi
wowote wa kuhamisha ubalozo wa Marekani kwenda Jerusalem au kuutambua
Jerusalem kuwa mji mkuu wa Isael,” mshauri wa Bw. Abbas, Majdi
al-Khalidi aliliambia shirika la AFP.Waziri wa mashauri ya nchi za
kigeni nchini Jardan ameonya Marekani kuhusu hatari ya kuutambua
Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
No comments :
Post a Comment