Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI) katika ziara yake ya kikazi ya
kutembelea Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam kujua changamoto
walizonazo za upatikanaji wa dawa na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja
katika ziara iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa
Ubongo Muhimbili (MOI), Respicious Lwezimula (kulia), akizungumza
katika kikao hicho.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (wa tatu kushoto),
akizungumza na viongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika ziara
hiyo.
Kikao kikiendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (wa nne kulia), akiwa na viongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI)
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amani Malima,
akizungumza na viongozi kutoka MSD. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD,
Laurean Bwanakunu na Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Celestine
Haule.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (katikati), akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Temeke baada ya kufanya nao mazungumzo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD), imepongezwa kwa kushinda tenda ya kununua dawa Jumuhiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
Pongezi
hizo zimetolewa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH), Profesa Lawrence Mseru
wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na timu
yake wakati wakiwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea Hospitali za
Mkoa wa Dar es Salaam kujua changamoto walizonazo za upatikanaji wa dawa
na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.
“Kwanza
tunawapongezeni MSD kwa kufikia hatua ya kununua dawa katika Jumuhiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) hii ni hatua ya kujivunia
kama nchi” alisema Profesa Mseru.
Mseru
aliongeza kuwa licha ya kuwepo changamoto ndogo ndogo MSD imejitahidi
katika huduma ya usambazaji wa dawa hapa nchini hivyo akaomba
ushirikiano baina yao uendelee kudumishwa ili kutoa huduma nzuri zaidi
ya kuwahudumia wananchi ukizingatia kuwa taasisi hizo zote zinafanya
kazi ya Serikali.
Akizungumza
katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,
Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI),Respicious
Lwezimula alisema kazi kubwa inayofanywa na MSD inapaswa kuungwa mkono
kwa kununua dawa na vifaa tiba.
“Tuna
kila sababu ya kuwaunga mkono hawa wenzetu kwa kununua vifaa tiba na
dawa kutoka kwao badala ya kununua kwenye maduka ya watu binafsi kikubwa
tunawaomba bei yao iwe tofauti kidogo” alisema Lwezimula.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amani Malima alisema
suala la manunuzi ya dawa na vifaa tiba linachangamoto kubwa lakini MSD
wamesaidia sana kuzipunguza kutokana na ushirikiano wanaofanya baina yao
na wateja wao hawana budi kupongezwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amewaomba wateja wao hao kufanya Maoteo
ya mahitaji yao sahihi na kuyawasilisha MSD kwa wakati kwa mujibu wa
sheria yaani tarehe 30 Januari kila mwaka,hasa dawa na vifaa tiba
vinavyonunuliwa kwa manunuzi maalumu.
Bwanakunu
alihimiza watoa huduma katika hospitali hizo kutambua jukumu walilonalo
katika usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa tiba kwa wananchi.
Akizungumza
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Temeke na Taasisi ya Tiba ya
Mifupa, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo Muhimbili (MOI),
Bwanakunu alisema anazitambua changamoto zilizopo za usambaji wa dawa na
vifaa tiba na kuwa MSD katika kukabiliana na changamoto hizo imepata
msaada wa magari 220 kutoka Global Fund ambayo yataboresha usambazaji
kutoka mara nne kwa mwaka hadi mara sita kwa mwaka.
Kuhusu
vifaa vya Manunuzi maalumu Bwanakunu amesema hospitali zikiwa zinaomba
kwa wakati mmoja ingerahisisha kuagiza vifaa hivyo mapema,badala ya kila
hospitali kuleta kwa wakati wake.
“Vifaa
hivi tunaagiza nje ya nchi na mchakato wake unachukua muda mrefu hivyo
tukipata oda mapema itatusaidia kupunguza changamoto hiyo ” alisema
Bwanakunu.
No comments :
Post a Comment