Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD), Victoria
Elangwa (kulia), akipokea tuzo ya mshindi wa pili Sekta za Umma katika
Tuzo ya Mwajiri Bora 2017 katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, akimkabidhi cheti cha ushiriki wa tuzo hizo Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu na Utawala wa Bohari ya Dawa (MSD), Victoria
Elangwa. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Anthony Mavunde.
Wafanyakazi wa MSD wakifurahia ushindi huo wakiwa na tuzo zao.
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya
Dawa (MSD) imeibuka kidedea kwa kuwa mshindi wa pili (2) kwa upande wa
Sekta za Umma katika tuzo ya Mwajiri Bora mwaka 2017 zinazoandaliwa na
Chama cha Waajiri nchini
( ATE).
Akizungumza
katika hafla ya utoaji tuzo hizo, Mgeni rasmi Waziri wa Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema
uanzishwaji wa vipengele vipya katika tuzo hizo unazipa fursa za kipekee
taasisi za serikali kupata nafasi ya kushiriki na kushinda.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Bi.Victoria Elangwa amesema tuzo
hiyo ni matokeo ya maboresho ya kiutendaji kwa MSD ambayo yanafanyika
kulingana na Mpango Mkakati wa MSD wa mwaka 2017 -2020.
Ameongeza
kuwa hatua hiyo ya MSD kupata tuzo ya Taasisi ya Umma inayofanya vizuri
ni motisha kwa wafanyakazi na MSD kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii
zaidi.
No comments :
Post a Comment