Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Watu wenye ulemavu ) Stella Ikupa,akimkabidhi mkurugenzi
wa raslimali watu wa TBL Group, David Magese, tuzo ya ushindi wa jumla
katika kipengele cha kuajiri na kukuza vipaji vya wafanyakazi kutoka
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) hafla ya tuzo hizo ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.(Kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania,Dk.Aggrey Mlimuka
5/8.Baadhi
ya wafanyakazi wa TBL Group wakishangilia mafanikio ya kampuni yao
katika ukumbi wa Mlimani City baada ya kampuni yao kuibuka kidedea
………………….
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) imepata tuzo kutoka Chama Cha Waajiri Tanzania
(ATE) ya utekelezaji vigezo vya Raslimali Watu kwa viwango vinavyotakiwa
na kuwa kinara katika kipengele cha kuwa na mazingira bora ya ajira ,
kuajiri wafanyakazi wenye vipaji na kuendeleza vipaji vyao .Mbali na
tuzo hii kwa kipindi cha miaka 2 mfululizo iliyopita iliibuka mshindi wa
jumla wa tuzo ya mwajiri bora nchini.
Hafla ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ya kutoa tuzo kwa makampuni kwa mbalimbali yanayokidhi viwango bora vya Raslimali
Watu katika vipengele mbalimbali vilivyowekwa na chama hicho ilifanyika
katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo mgeni Rasmi
alikuwa ni Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Kazi na Ajira,Vijana na
Walemavu,Mh.Jenesta Mhagama, aliyewakilishwa na Naibu Waziri wake ,Mh. Stella Ikupa, ambapo kampuni ya Coca-Cola iliibuka mshindi wa tuzo ya Mwajiri bora na kampuni ya Geita Gold Mine mshindi wa pili.
Akiongelea
ushindi wa tuzo hii,Mkurugenzi Raslimali Watu wa TBL Group,David
Magese,alisema kuwa ushindi huu ni heshima kubwa kwa kampuni kwa kuona
mchango inaoutoa kupitia uwekezaji wake unatambuliwa “Tuzo
za aina hii tunazoendelea kuzipata zinazidi kututia moyo na tuzo hii
sio ya kampuni bali ni ya wafanyakazi wote ,tunajivunia kuona kampuni
yetu inaongoza kwa kuwa na mazingira bora yanayovutia kufanyia kazi na tutaendelea kuyaboresha zaidi siku hadi siku”
Aliongeza
kusema kuwa kampuni inaendelea na mkakati wa kutoa mafunzo ya ndani na
nje kwa wafanyakazi wake kukuza ujuzi na vipaji vyao sambamba na mafunzo
ya ziada ambayo yanawasaidia katika maisha yao ya kila siku nje ya
sehemu ya kazi, kama
mafunzo yaliyoendeshwa kwa wafanyakazi wa kampuni ya jinsi ya kutumia
fedha zao kwa ufanisi badala ya kuzitumia bila mpangilio na mambo yasiyo
ya lazima.
Mbali
na mafunzo hayo alisema kuwa kampuni imekuwa na mpango wa kuwapatia
ujuzi wafanyakazi wake wanawake kupitia jukwaa lao la TBL Women’s
Forum,ambapo wananufaika kwa kupatiwa mafunzo ya mbinu za ujasiriamali
na kujadili jinsi ya kukabiliana na changamto mbalimbali zinazosababisha
wanawake kubaki nyuma.
No comments :
Post a Comment