Katibu Mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel.
………………………………………………………………….
Katibu Mkuu wizara ya viwanda,
biashara na uwekezaji, Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na Katibu mkuu
Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Prof Adolf Mkenda
wakutana na wawekezaji kutoka makampuni mbalimbali kwenye Mkutano wa
Kuvutia Uwekezaji uliofanyika Ubalozini nchini China.
Mkutano
huu umehudhuriwa na wawakilishi wa makampuni 100 yenye nia ya kuwekeza
Tanzania. Aidha wamekutana na Uongozi wa Benki ya AIIB iliyoanzishwa
kutoa mikopo kwa miradi ya miundombinu kwa nchi wanachama wa
Belt&Road. Benki hiyo imeikaribisha Tanzania kujiunga nayo ili iweze
kufaidika na fursa za mikopo nafuu.
Vilevile,
wamekutana na Uongozi wa Kampuni ya Hainan Group (H&A Group)
inayomiliki mashirika mbalimbali ya ndege na mahoteli. China imeeleza
kwamba katika miaka mitano ijayo itanunua bidhaa kutoka Nje ya nchi
zenye thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni 24 hivyo nchi za Afrika
zina fursa ya kunufaika na soko lake endapo zitajipanga.
Kwenye
mkutano huo China imeahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika
nyanja za uchumi hususan kwenye ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa
Bagamoyo SEZ.
Pia China imeeleza kwamba inaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kutekeleza miradi mingine ya ujenzi wa miundombinu.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika mkutano huo
Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Prof Adolf Mkenda
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika mkutano huo
No comments :
Post a Comment