Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa wananchi wa Kigwe alipofanya ziara
ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa soko la Kidwe Wilayani Bahi Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel
alipowalisi kukagua ujenzi wa Soko la mazao la Kigwe Lililopo Bahi
Dodoma.
Afisa Mtendaji Kata Bw. John
Mchiwa akikabidhi taarifa ya Ujenzi wa Soko Kigwe kwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana,
Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Bahi
kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel
akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa soko la Kigwe lililofadhiliwa na
Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za
Kifedha Vijijini (MIVARF) kwa kushirikiana na Halmashauri wakati wa
ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama
Wilayani Bahi Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi
Bi. Rachel Chuwa wakati wa ziara yake Kigwe.
Mratibu Taifa wa Programu ya
Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini
(MIVARF) Bw. Walter Swai akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Kigwe
walipotembelea Kijiji hicho kuona ujenzi wa soko la Kigwe unavyoendelea.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)
………………………………………………………………………….
Na. MWANDISHI WETU – DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
kuhakikisha inamaliza ujenzi wa soko la Kigwe kwa ...
kuhakikisha wanajenga
vyoo na vibanda vidogo vitakavyo saidia soko hilo lililojengwa na
Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za
Kifedha Vijijini (MIVARF).
Ameyasema hayo alipofanya ziara
yake Wilayani Bahi Novemba 21, 2017 kwa lengo la kujionea namna
uboreshaji wa soko hilo ambalo tayari limekamilika kwa asilimia 90 na
kukabiliwa na changamoto za vibanda na vyoo vya kudumu.
“Ninaiagiza Halmashauri hii
kuhakikisha inaleta timu ya wataalamu kupima viwanja na kuvigawa kwa
wananchi pamoja na kumalizia ujenzi wa Vyoo vya soko ili lianzae
utekelezaji wake haraka na kuhakikisha umeme unafungwa ndani ya soko
hili”.
Kwa upande wake Mbunge wa Bahi
Mhe. Omary Badwel alieleza ujenzi wa soko ni jambo ja muhimu linalogusa
wanakigwe wote kwani tangu enzi za mkoloni kumekuwa na changamoto ya
soko na kuwataka wananchi kulitunza na kuhakikisha linakuwa msaada kwao
wote.
“Soko hili toka utawala wa
mkoloni kulikuwa na soko bovu hivyo hatua ya kulikamilisha litavutia
wengi na kukuza uchumi wa wana Kigwe wote.”Alisisistiza Badwel
Kwa upande wake mkazi wa Kigwe
Bi.Anastazia Mkatato alieleza kuwa kujengwa kwa soko hilo litatatua
changamoto iliyopo ya kukosa soko la kudumu kwani yaliyopo ni madogo
yanayomilikiwa na watu binafsi.
“Ninaishukuru Ofisi ya Waziri
Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na
Huduma za Kifedha Vijijini iliyoamua kutujengea soko hapa Kigwe na hii
itatupa nafasi ya kuuza mazao na bidhaa kwa wingi kupelekea kukuza
uchumi wetu.”Alieleza Anastazia.
Naye Mratibu wa Mradi Taifa
Bw.Walter Swai alieleza kuwa soko hili ni muhimu kwa wana Kigwe na
maeneo jirani , hivyo tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuhakikisha
vifaa vinawekwa ikiwemo Meza za kuuzia mbidhaa sokoni.
“Tayari Ofisi yangu itachukua
changamoto hii ya kukosekana kwa meza za kuuzia na kuitatua ndani ya
mwezi mmoja hivyo niwaahidi kutekeleza haya.”Alisisitiza Bw.Swai
Ujenzi wa soko la Kigwe
umegharimu jumla ya zaidi ya shilingi milioni 68 ambapo Ofisi ya Waziri
Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na
Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) ilitoa kiasi cha zaidi ya shilingi
Milioni 50 pamoja na Mfuko wa jimbo kuchangia jumla ya shilingi Milioni
15. Dhumuni la mradi ni kuwa na eneo rasmi la kufanyia biashara na
kuwezesha wajasiliamali wa Kigwe na kujikwamua kiuchumi na kukuza
maendeleao yao
No comments :
Post a Comment