Waziri
wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akifyatua
bastola juu leo Jijini Dar es Salaam kuashiria Ufunguzi wa Mashindano ya Riadha
kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo nchini
Japan.
NA
SHAMIMU NYAKI-WHUSM
WANAWAKE
nchini wametakiwa kushiriki katika Michezo mbalimbali kwani ni fursa nzuri
ambayo inasaidia kupata ajira na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja pamoja na
kuitangaza nchi kama ambavyo wanafanya wanamichezo wakiume.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akizindua Mashindano ya Riadha
kwa wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo nchini Japan
ambapo amewataka wanawake waliopata fusa ya kushiriki katika mashindano hayo
kujituma zaidi na kujiamini ili wapate nafasi ya kushiriki katika Olimpiki hiyo
na kuiletea heshima Nchi yetu.
“Leo
vitaibuka vipaji vingi vitakavyosaidia nchi yetu kupiga hatua katika mchezo wa
Riadha,nawaasa mjitume zaidi muwe na nidhamu pamoja na kujiamini ili mfanye vizuri katika mashindano haya hatimaye mpate nafasi ya kushiriki
Olimpki ya mwaka 2020 kule nchini
Japan”.Alisema Mhe. Mwakyembe.
Aidha
amewataka waamuzi wa mchezo huo kutumia vizuri taaluma yao kwa kufuata
Sheria,taratibu na kanuni walizofundishwa na kutii kiapo walichoapa katika
kuchezesha mchezo huo kwa kutoa matokeo sahihi na kwa wakati ili kuepusha
manung’uniko.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Juliana Shonza amesema Serikali ipo
tayari kutoa ushirikiano kwa wanamichezo wote ambao wapo tayari na wanashiriki
katika michezo mbalimbali kwani nia ya Serikali ni kukuza na kuendeleza Michezo
hapa nchini.
“Ni
fursa ya pekee kwenu vijana na wanawake kwa ujumla kutumia nafasi hii kuonyesha
uwezo wenu katika michezo hii ili mpate nafasi ya kushiriki mashindano
malimbali duniani na hatimaye mpate ajira itakayowezesha kutengeneza maisha
yenu ya baadae.”Alisisitiza Mhe.Shonza.
Naye
mwanariadha wa mbio za mita mia Bi. Winifrida Makenji kutoka Shule ya Sekondari
Makongo ya Jijini Dar es Salaam ambaye ameingia katika fainali itakayochezwa
hapo kesho amesema sifa kubwa ya yeye kufikia hatua hiyo ni kujiamini,kufanya
mazoezi pamoja na kufuata maelekezo ya mwalimu.
Mashindano
hayo yaliyofadhiliwa na Kampuni ya Ushirikiano ya Japan (jicA) yamehusisha
michezo ya Riadha,kurusha mikuki pamoja na Kisahani ambapo yatamalizika kesho
katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Habari Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza leo Jijini Dar
es Salaam katika Ufunguzi wa Mashindano
ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo nchini
Japan.Kulia ni Waziri wa Wizara hiyo
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri
wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimpongeza
mshindi wa kurusha kisahani Bi. Mwanjala Abdala kutoka Dodoma wakati wa
Mashindano ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020
yatakayofanyika Tokyo nchini Japan yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Habari Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akimvalisha Medali ya
ushindi mshindi namba mbili wa kurusha kisahani leo Jijini Dar es Salaam katika
Mashindano ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020
yatakayofanyika Tokyo nchini Japan.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la
Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja.
Waziri
Mhe.Dkt Mwakyembe na Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza wa Wizara ya Habari Sanaa
na Michezo wakimvalisha medali ya ushindi mshindi namba moja wa kurusha
kisahani Bi.Joyce Barnabas kutoka Dodoma leo Jijini Dar es Salaam katika
Ufunguzi wa Mashindano ya Riadha kwa Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020
yatakayofanyika Tokyo nchini Japan.
Waziri
Mhe.Dkt Mwakyembe na Naibu Waziri Mhe.Juliana Shonza wa Wizara ya Habari Sanaa
na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo pamoja na wafadhili
kutoka kampuni ya jiCA ya nchini Japan wanaoshiriki Mashindano ya Riadha kwa
Wanawake kuelekea Olimpiki ya mwaka 2020 yatakayofanyika Tokyo Nchini Japan
yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.Wa pili kushoto waliokaa ni
Balozi wa Japan hapa nchini Mhe.Masahran Yoshida.
NA
ISMAIL NGAYONGAMAELEZO
WAFANYABIASHARA na Wajasiriamali Wanawake nchini
wametakiwa kuwa na uthubutu wa kutenda na kufikia malengo waliyojiwekea kwa
kutumia fursa zilizopo ili kujiletea maendeleo ya kiuchumi katika jamii
inayowazunguka.
Wito
huo huo umetolewa (juzi) Novemba 23, 2017 Jijini Dar es Salaam na Afisa
Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mwajuma Magwiza
wakati wa mkutano wa Jukwaa la Mwanamke Mjasiriamali na Ubunifu liliondaliwa na
Taasisi ya Dominion Leadership Connect.
Magwiza
alisema Wanawake ndio kundi kubwa katika jamii ya Watanzania na wanapaswa
kutambua kuwa hakuna njia ya mkato katika kuyafikia mafanikio yao kiuchumi na
badala yake wajihangaishe katika kutatua changamoto zilizopo ili kupata
mafanikio katika shughuli mbalimbali za kila ikiwemo biashara na ujasiriamali..
“Serikali
imefungua milango ya ushirikiano kwa kuanisha fursa za kujikwamua kiuchumi kwa
Wafanyabiashara na Wajasiriamali wanawake, zipo taratibu zilizoanishwa katika
kuzifikia fursa hizo na hivyo ni wajibu wetu kuachana na mazoea ya utamaduni
ulijiongezeka katika jamii yetu” alisema Magwiza.
Kwa
mujibu wa Magwiza alisema Serikali inatambua changamoto mbalimbali
zinazowakabili Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake nchini ikiwemo ukosefu
wa mtaji ya biasharara, ambapo hata hivyo halmashauri mbalimbali nchini
zimeanza kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kutenga asilimia 5 ya bajeti zao
kwa ajili ya kusaidia vikundi vya Wanawake na Vijana.
Aidha
Magwiza aliwataka Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake kutambua kuwa mtaji
sio kigezo cha kukwama katika kujiletea maendeleo yao na badala yake watumie
majukwaa yao kuwa chachu ya mabadiliko ya kifikra na hatimaye kufikia malengo
waliyojiwekea.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya GIBR FARM, Hadija Jabir alisema
safari ya mabadiliko ya kiuchumi kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake nchini
itapata mafanikio makubwa iwapo jamii hiyo itaunganisha nguvu ya pamoja katika
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowazunguka.
Aliongeza
kuwa ili mafanikio hayo yaweze kupatikana ni wajibu wa Wafanyabiashara na
Wajasiriamali Wanawake walielezane ukweli na uwazi uliopo katika kubaini fursa
na kutumia rasilimali zilizopo ili ziweze kuwaletea maendeleo ya haraka.
“Safari
ya kujikwamua kiuchumi huwa ngumu katika ngazi za awali, kwa upande wetu
kampuni ya GIBR FARM inayojihusisha na uzalishaji wa mbogamboga na matunda, tumefanikiwa
kupanua wigo wa soko na sasa tunauza bidhaa zetu katika nchi za Sweden, Italy
na Ujerumani” alisema Hadija.
Naye
Mwanzilishi wa Kampuni ya uzalishaji kuku ya GOKUKUZ, Bulla Boma alisema
kumekuwepo na changamoto ya fursa za masoko katika mauzo ya bidhaa kwa
Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake hususani waliopo katika mfumo usio
rasmi, hatua inayowafanya wengi wao kukatishwa tamaa wakiwa katika ngazi za
awali.
Hata
hivyo alisema kutokana na kupanua wigo wa ushirikano na mawasiliano na
Wafanyabishara na Wajasiriamali wakubwa waliopo nchini, kampuni yake kwa sasa imejiwekea
malengo ya kupanua wigo wa bidhaa hiyo katika soko la kimataifa.
Kongamano
hilo lilibeba kauli mbiu ya “Mwanamke Mjasiriamali na Ubunifu” lililenga katika
kuhamasisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali wanawake nchini kuibua na kutumia
fursa za kiuchumi ili kuweza kuwaletea maendeleo yao katika jamii.
|
Mmoja wa wawezeshaji wa mkutano wa
jukwaa la Wajasiriamali na Wafanyabiashara Wanawake ulioandaliwa na Taasisi ya Dominion
Leadership Connect akizungumza na wajumbe wa jukwaa lililofanyika Novemba 23,
2017 Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kuwajengea uwezo
Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake kukabiliana na changamoto mbali
katika fursa za kiuchumi.
Baadhi
ya Wafanyabiashara na Wajasirimali Wanawake wakifuatilia mkutano wa jukwaa la
Wajasiriamali na Wafanyabiashara Wanawake ulioandaliwa na Taasisi ya Dominion
Leadership Connect lililolenga kuwajengea uwezo na Wajasiriamali wa kukabiliana
na changamoto mbali katika fursa za kiuchumi. Mkutano huo ulifanyika Novemba 23
2017
Baadhi
ya Wafanyabiashara na Wajasirimali Wanawake wakifuatilia mkutano wa jukwaa la
Wajasiriamali na Wafanyabiashara Wanawake ulioandaliwa na Taasisi ya Dominion
Leadership Connect lililolenga kuwajengea uwezo na Wajasiriamali wa kukabiliana
na changamoto mbali katika fursa za kiuchumi. Mkutano huo ulifanyika Novemba 23
2017.
Mwanzilishi wa Tamasha la
Nyamachoma, Carol Ndosi akizungumza na Wajasiriamali na Wafanyabiashara
Wanawake wakati wa mkutano wa jukwaa la Wafanyabiashara Wanawake lililoandaliwa
na Taasisi ya Dominion Leadership Connect lililofanyika Novemba 23, 2017 Jijini
Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kuwajengea uwezo Wafanyabiashara na
Wajasiriamali Wanawake kukabiliana na changamoto mbali katika fursa za
kiuchumi.
Afisa Maendeleo ya Jamii katika
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mwajuma Magwiza akuzungumza na Wajasiriamali
na Wafanyabiashara Wanawake wakati wa mkutano wa jukwaa la Wafanyabiashara
Wanawake lililoandaliwa na Taasisi ya Dominion Leadership Connect lililofanyika
jana Novemba 23, 2017 Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kuwajengea
uwezo Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake kukabiliana na changamoto mbali
katika fursa za kiuchumi.(PICHA NA MPIGA
PICHA WETU)
No comments :
Post a Comment