Mmoja wa wawezeshaji wa mkutano wa
jukwaa la Wajasiriamali na Wafanyabiashara Wanawake ulioandaliwa na
Taasisi ya Dominion Leadership Connect akizungumza na wajumbe wa jukwaa
lililofanyika Novemba 23, 2017 Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo
ulilenga kuwajengea uwezo Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake
kukabiliana na changamoto mbali katika fursa za kiuchumi.
Afisa Maendeleo ya Jamii katika
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mwajuma Magwiza akuzungumza na
Wajasiriamali na Wafanyabiashara Wanawake wakati wa mkutano wa jukwaa la
Wafanyabiashara Wanawake lililoandaliwa na Taasisi ya Dominion
Leadership Connect lililofanyika jana Novemba 23, 2017 Jijini Dar es
Salaam. Mkutano huo ulilenga kuwajengea uwezo Wafanyabiashara na
Wajasiriamali Wanawake kukabiliana na changamoto mbali katika fursa za
kiuchumi.
Mwanzilishi wa Tamasha la
Nyamachoma, Carol Ndosi akizungumza na Wajasiriamali na Wafanyabiashara
Wanawake wakati wa mkutano wa jukwaa la Wafanyabiashara Wanawake
lililoandaliwa na Taasisi ya Dominion Leadership Connect lililofanyika
Novemba 23, 2017 Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kuwajengea
uwezo Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake kukabiliana na
changamoto mbali katika fursa za kiuchumi.
Mgeni rasmi katika mkutano wa
jukwaa la Wajasiriamali na Wafanyabiashara Wanawake, Afisa Maendeleo ya
Jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mwajuma Magwiza akiwa
katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa jukwaa hilo mara baada ya
kumalizika ikwa mkutano huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 23,
2017
NA MPIGAPICHA WETU
………….
Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
DAR ES SALAAM
WAFANYABIASHARA na Wajasiriamali
Wanawake nchini wametakiwa kuwa na uthubutu wa kutenda na kufikia
malengo waliyojiwekea kwa kutumia fursa zilizopo ili kujiletea maendeleo
ya kiuchumi katika jamii inayowazunguka.
Wito huo huo umetolewa (juzi)
Novemba 23, 2017 Jijini Dar es Salaam na Afisa Maendeleo ya Jamii katika
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mwajuma Magwiza wakati wa mkutano
wa Jukwaa la Mwanamke Mjasiriamali na Ubunifu liliondaliwa na Taasisi
ya Dominion Leadership Connect.
Magwiza alisema Wanawake ndio
kundi kubwa katika jamii ya Watanzania na wanapaswa kutambua kuwa hakuna
njia ya mkato katika kuyafikia mafanikio yao kiuchumi na badala yake
wajihangaishe katika kutatua changamoto zilizopo ili kupata mafanikio
katika shughuli mbalimbali za kila ikiwemo biashara na ujasiriamali..
“Serikali imefungua milango ya
ushirikiano kwa kuanisha fursa za kujikwamua kiuchumi kwa
Wafanyabiashara na Wajasiriamali wanawake, zipo taratibu zilizoanishwa
katika kuzifikia fursa hizo na hivyo ni wajibu wetu kuachana na mazoea
ya utamaduni ulijiongezeka katika jamii yetu” alisema Magwiza.
Kwa mujibu wa Magwiza alisema
Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wafanyabiashara
na Wajasiriamali Wanawake nchini ikiwemo ukosefu wa mtaji ya biasharara,
ambapo hata hivyo halmashauri mbalimbali nchini zimeanza kutekeleza
maelekezo ya Serikali ya kutenga asilimia 5 ya bajeti zao kwa ajili ya
kusaidia vikundi vya Wanawake na Vijana.
Aidha Magwiza aliwataka
Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake kutambua kuwa mtaji sio kigezo
cha kukwama katika kujiletea maendeleo yao na badala yake watumie
majukwaa yao kuwa chachu ya mabadiliko ya kifikra na hatimaye kufikia
malengo waliyojiwekea.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya GIBR FARM, Hadija Jabir alisema safari ya mabadiliko
ya kiuchumi kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake nchini itapata
mafanikio makubwa iwapo jamii hiyo itaunganisha nguvu ya pamoja katika
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowazunguka.
Aliongeza kuwa ili mafanikio hayo
yaweze kupatikana ni wajibu wa Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wanawake
walielezane ukweli na uwazi uliopo katika kubaini fursa na kutumia
rasilimali zilizopo ili ziweze kuwaletea maendeleo ya haraka.
“Safari ya kujikwamua kiuchumi
huwa ngumu katika ngazi za awali, kwa upande wetu kampuni ya GIBR FARM
inayojihusisha na uzalishaji wa mbogamboga na matunda, tumefanikiwa
kupanua wigo wa soko na sasa tunauza bidhaa zetu katika nchi za Sweden,
Italy na Ujerumani” alisema Hadija.
Naye Mwanzilishi wa Kampuni ya
uzalishaji kuku ya GOKUKUZ, Bulla Boma alisema kumekuwepo na changamoto
ya fursa za masoko katika mauzo ya bidhaa kwa Wafanyabiashara na
Wajasiriamali Wanawake hususani waliopo katika mfumo usio rasmi, hatua
inayowafanya wengi wao kukatishwa tamaa wakiwa katika ngazi za awali.
Hata hivyo alisema kutokana na
kupanua wigo wa ushirikano na mawasiliano na Wafanyabishara na
Wajasiriamali wakubwa waliopo nchini, kampuni yake kwa sasa imejiwekea
malengo ya kupanua wigo wa bidhaa hiyo katika soko la kimataifa.
Kongamano hilo lilibeba kauli mbiu
ya “Mwanamke Mjasiriamali na Ubunifu” lililenga katika kuhamasisha
Wafanyabiashara na Wajasiriamali wanawake nchini kuibua na kutumia fursa
za kiuchumi ili kuweza kuwaletea maendeleo yao katika jamii.
No comments :
Post a Comment