
Na Mathias Canal, Singida
Mfuko
wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa Hiari (PSS)
umeendelea kuyafikia makundi mbalimbali kujiunga na mpango huo ambapo
pamoja na mambo mengine umeendelea kusaidia jamii ikiwa ni pamoja na
kuunga mkono juhudi za serikali.
Mapema
Leo asubuhi Novemba 25, 2017 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu amekabidhiwa mabati 100 na Meneja Uendeshaji wa Mfuko wa
Penseni (PSPF) Mkoani Singida Bi Hafsa Ally kwa niaba ya Mkurugenzi
Mkuu wa mfuko huo.
Mabati
hayo yametolewa na PSPF Kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Uongozi wa
Wilaya ya Ikungi inayoongozwa na Mhe Mtaturu katika kuimarisha mfuko wa
elimu kwa muktadha wa kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kuhimiza
utatuzi wa Changamoto mbalimbali katika Wilaya ya Ikungi ikiwemo
Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu,
Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.
Akizungumza
katika dhifa ya makabidhiano ya mabati hayo iliyofanyika katika eneo la
shule ya sekondari Ikungi Mhe Mtaturu ambaye pia ni mlezi wa mfuko wa
Elimu amewasihi wananchi na wadau kuchangia fedha au thamani zozote
kadri wawezavyo ili kufanikisha kuboresha miundombinu ya elimu katika
wilaya hiyo.
Sambamba
na hayo pia ameushukuru Uongozi wa Mfuko wa Penseni PSPF kwa kuunga
mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika
kuboresha elimu kwa manufaa ya watanzania wote.
Aidha,
ameupongeza mfuko huo wa PSPF kwa mpango wao wa uchangiaji wa hiari
ambapo mwanachama hutakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 , ili kuwa
huru kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake ambapo kiwango
cha chini kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia
kupitia benki.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, Meneja Uendeshaji wa Mfuko
wa Pensheni (PSPF) Mkoani Singida Bi Hafsa Ally Ameeleza kuwa PSPF ipo
karibu na watumishi lakini pia ipo karibu na jamii hivyo wamempongeza
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuwashirikisha kwenye jambo hilo muhimu la
kuboresha elimu katika wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla wake.

No comments :
Post a Comment