
Jonas Kamaleki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara kuweza
katika viwanda vya madawa ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa
bidhaa hiyo nchini.
Rais Magufuli ameto wito huo leo
nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wakati akizindua Hospitali ya
Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Syansi Shirikishi Muhimbili.
“Wafanyabiashara tumieni fursa hii
ili muweze ...
kuwekeza katika viwanda vya madawa kwani Tanzania imepewa
nafasi ya kuuza dawa katika nchi za SADC na tumetenga zaidi ya bilioni
miambili kwa ajili ya kununulia madawa,”amesema Rais Magufuli.
Ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya kujenga kiwanda cha madawa Mloganzila badala ya kukkopesha fedha
hizo kwa watu wanaojenga nmajumba.
Magufuli amesema kuwa Serikali
imedhamira kuwekeza katika masuala ya Afya ili kuwa na Taifa lenye watu
wenye afya ili wawezekushiriki katika ujenzi wa viwanda. Bila afya njema
hakuna ambacho kitafanyika, alisisitiza Rais Magufuli.
Katika Chuo kitakachojengwa
Mloganzila kikitumika apmoja na hospitali hiyo, Rais Magufuli amesema
kitatola wataalaam wenye ubora ambao utaendana na hadhi ya chuo hicho.
Ili kuongeza ufanisi katika
hospitali za mikoa, Rais ameshauri zisimamiwe na wizara ya afya kuliko
ilivyo sasa ambapo zilikuwa zikisimamiwa na Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
“Hospitali hizo haziwezikusimamiwa
na watu ambao sio wataalaamu wa tiba, hivyo hospitali zote za mikoa
ziwe chini ya wizara ya Afya ambayo ndiyo inasimamia Sera ya Afya, na
hizo nyingine za wilaya, kata na vijiji ndizo zisimamiwe na TAMISEMI,
alisema Rais Magufuli.
Amesema kwa usimamizi huo sekta ya Afya itaimarika kuanzia ngazi ya mikoa hadi Taifa.
Rais Magufuli amewataka madaktari
na wahudu wa afya hapo katika Hospitali ya Mloganzila kutunza vifaa na
miundombinu ya hospitali hiyo ili kuhakikisha ubora uliopo sasa hivi
uweze kudumu.
Amewataka kutoharibu vifaa hivyo
vya kisasa ambavyo Rais amesema kuwa Hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa
na ina hadhi kama hospitali za Ulaya.
Kwa upande wa Bima za Afya, Rais
magufuli amewataka wananchi kujiunga na mifuko ya bima ya afya ambayo
itawahakikishia upatikanaji wa matibabu.
“Msiendekeze ununuzi wa nguo,
starehe bali changieni katika mifuko hiyo ambayo itawasaidia watoto wenu
kupata matibabu ya uhakika, ukiuza majogoo wawili utaweza kumlipia
mwanao gharama za matibabu kwa mwaka,”alisisitiza Rais Magufuli.
Aidha, Rais amewataka mawaziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia kushirikiana katika kuendesha hospitali za
Muhimbili na Mloganzila.
Amewambia kuwa umimi hauhitajiki
katika masuala ya kitaifa hivyo wizara hizo zishirikiane katika
kuhakikisha ufanisi wa Hospitali ya Mloganzila.
Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu
wa Chuo cha Afya ya Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Apolinary
Kamuhabwa amesema kuwa Hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa ambavyo
vitatumika katika kutoa huduma za tiba ya dhararula kwa watu wazima na
watoto, huduma za magonjwa ya akina mama na mfumo wa uzazi, magonjwa ya
macho, mfumo wa pua, koo na masikio na magonjwa ya akili.
Kwa mujibu wa Prof. Kamuhabwa
huduma nyingine zitakazotolewa na hospitali hiyo ni pamoja na hmatibabu
ya magonjwa ya mifupa na majeruhi, upasuaji mkubwa na mdogo, huduma za
kusafisha damu kwa magonjwa ya figo na tiba za magonjwa mbalimbali
zikiwemo za kinywa.
Hospitali ya Mloganzila imejengwa
na Serikali ya Tanzania na Korea ya Kusini ambayo imetoa mkopo wa
masharti nafuu. Ujenzi wa Hospitali umegharimu jumla ya Dola za
Kimarekani milioni 94.5 (USD) ambapo Serikali ya Tanzania imetoa jumla
ya dola za Kimarekani milioni 18.4.
No comments :
Post a Comment