Dr. Noam Koriat akitoa mafunzo kwa
watumishi wa Wizara ya Utalii na Taasisi zake katika ukumbi wa mikutano
wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi wakimsikiliza Dkt. Wakati wa mafunzo.
…………..
Ziara ya kutembelea nchi ya
Israel iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania na kuhususisha viongozi
wa Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza kuzaa matunda ambapo mtaalamu
wa mfumo wa mawasiliano Kutoka Israel, Dkt Norma Kortiat amewasili
nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo yanayohusiana na jinsi ya kutangaza
utalii wa Tanzania kwa njia ya kidigitali “Digital Marketing”. Mafunzo
haya yanategemewa kuwawezesha watumishi kuongeza ufanisi kwa wa kutumia
teknologia mpya katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.
Mafunzo haya ya siku mbili
yameanza leo tarehe 21-22 yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam ambayo yanahudhuriwa na
watumishi Kutoka Idara ya Utalii , Bodi ya Utalii, Mamlaka ya Wanyama
Pori,Mamlaka ya Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro, Wakala
wa Huduma za Misitu na kamisheni ya Utalii Zanzibar.
No comments :
Post a Comment